Ashangaza kuwaletea wenzake viungo vya mikono
CHARLES WANYORO na FAUSTINE NGILA
Maafisa wa kituo cha polisi cha Kabachi walishangazwa na mwanaume mmoja aliyekatwa mikono baada ya kurudi na viungo vya mikono na kuwaomba wenzake waviweke kama ushahidi.
Bw Samuel Ndutuwa miaka 40 aliseambia polisi kwamba alishambuliwa na nduguye Josedph Ngolua Jumanne asubuhi kwenye mzozo wa shamba na walikuwa anataka waweke mabaki ya mikono huo kama Ushahidi.
Alikuwa ameufunga kwa kipande cha nguo na kuuweka kwenye mfuko wa koti lake.
Bw Ndutu alisema kwamba alishambuliwa alipokuwa akienda kuangalia shamba lake la miraa kijiji cha Leeta ,Igembe Kaskazini.
Ata baada ya kuvunja damu sana alikuwa taratibu akiwaeleza maafisa hao wapolisi huku wakirekodi kwenye kitabu cha matukio.Aliweka mkono kwenye mfuko na kuchua baki la mkono.
Akielezea hayo kwenye hospitali ya kaunti ndogo ya Mutuati alipokuwa ameenda kuchukua P3 Bw Ndutu alisema kwamba ndunguye alianza kutetesha na kumkabilia kuhusiana na maswala ya ardhi .
Alimkibiza na alipomshika akamkata mkono njuu ya kifundo cha mkono.
Bw Ndutu aliomba polisi wamkamate ndunguye aliyenda mafichoni baada ya kutenda kitendo hicho cha unyama.