• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Bungoma yamulikwa tena kwa matumizi ovyo ya fedha

Bungoma yamulikwa tena kwa matumizi ovyo ya fedha

 DENNIS LUBANGA na CECIL ODONGO

MDHIBITI Mkuu wa bajeti za serikali alimulika kaunti ya Bungoma kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi wakati wa mwaka wa kifedha 2017/18 na kupandisha gharama ya matumizi ya pesa za kaunti.

Kulingana na ripoti ya mdhibiti mkuu wa bajeti Agnes Odhiambo, kuongezeka kwa idadi ya wafanyakazi katika kaunti hiyo kulipandisha gharama ya kulipa mishahara kwa asilimia 35 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, hatua iliyotajwa kama matumizi mabaya ya fedha za umma.

Ripoti hiyo inafafanua kwamba wafanyakazi wa ziada walipandisha gharama ya kulipa mishahara hadi Sh4.6 milioni katika mwaka wa kifedha 2017/18 kutoka kwa Sh3.42 bilioni mwaka wa kifedha 2016/17.

“Gharama ya juu ya mshahara iliongezeka kwa asilimia 35.5 kutoka kwa Sh3.42bilioni mwaka wa kifedha 2016/17 hadi Sh4.63bilioni mwaka uliofuatia,” ikaandika katika ripoti hiyo.

Matumizi ya fedha katika ziara za ndani na nje ya nchi yalifikia Sh183.42milioni huku mawaziri na gavana wakitumia Sh168.4 kati ya hela hizo nalo bunge la kaunti likitumia Sh15.02milioni zilizosalia.

Hata hivyo kiwango hicho kilikuwa cha chini kikilinganishwa na mwaka wa 2016/2017 ambapo Sh351milioni zilitumika kugharamia safari hizo.

Ripoti hiyo vile vile ilifichua kwamba fedha nyingi za kaunti zilielekezwa katika ulipaji wa mishahara na mambo yasiyo na umuhimu badala ya kutumika kwenye miradi ya maendeleo ya kuwanufaisha wananchi.

  • Tags

You can share this post!

Ngono ni muhimu sana katika maisha ya uzeeni, aeleza ajuza

Habibu alinitema baada ya kuugua, alia mwanamitindo

adminleo