Chakwera ashinda tena katika marudio ya uchaguzi
AFP na FAUSTINE NGILA
Kiongozi wa upizani nchini Malawi Lazarus Chakwera alishinda uchanguzi wiki iliyopita baada ya kurudiwa kwa uchaguzi wa urais huku akipata asilimia 58.57 ya kura tume ya uchanguzi ilisema Jumamosi.
Peter Mutharika aliyeshinda mwaka uliopita Mei 2019 alipata pigo baada ya ushindi wake kufutwa na korti iliyoamuru ushindi huo ulikuwa na udanganyifu.
Wapigaji kura milioni 6.8 walirudi kupiga kura Jumanne. Mwenyekiti wa tume ya uchanguzi Chifundo Kachale aliambia wanahabari.
Tume hiyo ilitangaza Lazarus Chakwera mshindi huku akijizolea asilimia 58.8 ya kura na kutawazwa rasmi kama Rais wa Malawi.
Peter Mutharika alipata kura 1,751,377 huku Peter Dominico Kuwani akipata kura 32,456. Wapiga kura walijitokeza kwa asilimia 68.81.
Matangazo hayo yalipokelewa kwa shwange na deremo huku wafuasi wa upizani wakipepersha bendera ya taifa ya Malawi yenye rangi nyekundu ,nyeusi na kijani kibichi.
Februari serikali ya Malawi iligundua kwamba uchaguzi uliofanyika mwaka uliopita ulikuwa umekubwa na udanganyifu.
“Huu ni ushindi kwa watu wa Malawi na demokrasia na haki,” alisema Chakwera baada ya kutangazwa mshindi.
“Huu ni ushidi ambao utasaidia kujenga Malawi mpya ambapo kila mtu atahusiswa.”