TAIFA LEO Logo
  • Habari
    • Habari za Kitaifa
    • Habari za Kaunti
    • Kimataifa
  • Siasa
  • Maoni
  • Makala
    • Afya na Jamii
    • Lugha, Fasihi na Elimu
    • Akili Mali
    • Jamvi La Siasa
    • Shangazi Akujibu
    • Bambika
    • Pambo
    • Dimba
  • Dondoo
  • Bi Taifa
  • Mashairi
  • Michezo
  • NIE Shuleni
Habari Mseto

Chungeni msilipukiwe na gesi, Kuria aonya polisi Kiandutu

February 3rd, 2024 Kusoma ni dakika: 1
  • Shiriki mitandao ya kijamii:
  • Facebook
  • X
  • LinkedIn
  • Email
  • WhatsApp

NA MWANGI MUIRURI

WAZIRI wa Utendakazi wa Umma Moses Kuria amedai kwamba kuna kiwanda haramu cha gesi katika Kaunti ya Kiambu kinachohudumu karibu na kituo cha polisi.

Amedai kwamba kiwanda hicho alichosema kiko katika mtaa wa Kiandutu, kiko katika hatari ya kulipuka kwa wakati wowote na walio katika hatari kuu, ni maafisa wa polisi walio na afisi zao hapo karibu.

Aliongeza kwamba kituo hicho cha gesi hakina usajili wowote wa kisheria na kwamba ni haramu, ni hatari na hivyo kinafaa kuhalalishwa au kufungwa.

Soma Pia: Embakasi: Nema yatimua maafisa wanne kwa kutoa leseni tata

Wenyeji katika mtaa huo wa viunga vya mji wa Thika waliambia Taifa Leo kwamba kiwanda hicho huambatana na ukora mwingi sana hata wa kushambuliana kwa bunduki.

“Ni kiwanda cha kipekee. Mara kwa mara huwa kunazuka vita vya ufyatuliamaji risasi katika barabara ya kuingia na kutoka kiwandani humo,” akasema jirani wa kiwanda hicho.

Kiwanda cha gesi cha Kiandutu ambacho Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria amekimulika. PICHA | MWANGI MUIRURI

Hayo yanajiri huku Rais William Ruto akitoa msimamo mkali dhidi ya mamlaka za kutoa leseni kwamba wote watakaonaswa katika mtandao wa ufisadi, utepetevu na uzembe unaohatarisha maisha ya watu, watakamatwa, wafutwe kazi na kutupwa jela.

Hii ni baada ya kiwanda katika mtaa wa Embakasi kulipuka na kusababisha vifo vya watu watatu huku zaidi ya 300 wakipata majeraha.

[email protected]

Mfanyakazi wa Khalwale kuzikwa Jumatatu
  • Facebook
  • Twitter
  • LinkedIn
  • Email
  • WhatsApp
Maiti ya kitoto malaika yatupwa karibu na ofisi ya umma

Habari Mseto Zaidi

Mkulima alia kufidiwa Sh3,000 kwa uharibifu wa Sh800,000...

June 16th, 2025

Korti yaruhusu madalali kuvamia makazi ya mbunge kufuata...

June 11th, 2025

Fyata mdomo, Sakaja amfokea Atwoli kwa kukosoa mabadiliko...

June 8th, 2025

Orengo sasa akunja mkia, aelekea Ikulu kuomba miradi ya...

June 5th, 2025

Habari Za Sasa

Jacob Ocholla Mwai apambana kurithi mali ya Kibaki

June 23rd, 2025

DPP kukata rufaa uamuzi ulioachilia huru Rose Njeri

June 23rd, 2025

Joto lapanda siku mbili kabla maandamano ya kuadhimisha...

June 23rd, 2025

Mzee aliyeondoka nyumbani 1965 na kwenda Uganda arejea...

June 23rd, 2025

KenyaBuzz

Shadow Force

Kyrah and Isaac were once the leaders of a multinational...

BUY TICKET

Thunderbolts*

After finding themselves ensnared in a death trap, seven...

BUY TICKET

The Accountant 2

When an old acquaintance is murdered, Wolff is compelled to...

BUY TICKET

Kiota School PTA Mothers day brunch

Theme: Mum Unplugged.Dress Code: A Symphony of Cultures.

BUY TICKET

Urembo

BUY TICKET

The Trial of Dedan Kimathi

From Stuart Nash, the Director of the multi-award-winning I...

BUY TICKET
TAIFA LEO Logo

Mitandao ya kijamii

Maarufu sana

Waiguru aweka kando ukuruba wake na Ruto, aishambulia serikali

June 20th, 2025

Familia ya Ojwang yataka ilindwe ikisaka haki kwa mpendwa wao

June 18th, 2025

Maandamano yazuka tena Nairobi

June 17th, 2025

Usikose

Jacob Ocholla Mwai apambana kurithi mali ya Kibaki

June 23rd, 2025

DPP kukata rufaa uamuzi ulioachilia huru Rose Njeri

June 23rd, 2025

Joto lapanda siku mbili kabla maandamano ya kuadhimisha Juni 25

June 23rd, 2025
Copyright © 2025 Nation Media Group. All rights reserved.