• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 9:55 AM
Corona: Karua aikosoa serikali

Corona: Karua aikosoa serikali

Na MAGDALENE WANJA

KIONGOZI wa chama cha Narc-Kenya Martha Karua ameikemea serikali kwa hatua yake ya kuruhusu raia wa China humu nchini wakati hofu imetanda kuhusu homa ya Corona ambayo asili yake ni China.

Kulingana na Bi Karua, serikali imeoyesha kulegea katika kuwajali Wakenya na badala yake kuhatarisha maisha yao.

“Huku vituo vya afya vya umma vikiendelea kutoa huduma katika hali duni, serikali inahatarisha maisha zaidi kwa kuiweka anga ya Kenya wazi kwa ndege za kutoka sehemu mbalimbali kama vile China,” akasema Bi Karua.

Aliilaumu serikali kwa kutojali wananchi kutokana na uhusiano wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili na kuwaweka katika hatari ya maambukizi ya Corona.

Bi Karua pia aliitaka serikali kufanya upesi kuwaleta wanafunzi wa asili ya Kenya ambao wamekwama nchini China kutokana na agizo la kuzuia uenezaji zaidi wa ugonjwa huo.

“Serikali ina jukumu la kuwatoa wanafunzi hao nchini China na kuwaleta nchini ambapo wanaweza kufanyiwa karantini,” akasema Bi Karua.

You can share this post!

Echesa aendelea kuandamwa na madai ya uhalifu

Kocha Ouma ataja kikosi cha Harambee Starlets kinachoelekea...

adminleo