• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
CORONA: Utalii kuathirika zaidi

CORONA: Utalii kuathirika zaidi

Na GEOFFREY ONDIEKI

[email protected]

Sekta ya utalii katika kaunti ya Samburu ndio imeathirika zaidi kutokana na mkurupuko was virusi vya corona.

Sekta ya utalii ndio huchangia mapato zaidi katika kaunti ya Samburu ambayo imekumbatia utamaduni.

Inahofiwa kuwa wafanyikazi mbalimbali ambao hutegemea sekta hiyo katika kaunti ya Samburu huenda wakapoteza kazi kutokana na ukosefu wa watalii.

Ijumaa iliyopita, halmashauri ya Utalii duniani WTTC ilitangaza kuwa huenda zaidi ya wafanyikazi milioni 50 wakapoteza nafasi za kazi kutokana janga la virusi vya Corona.

Nchi ambazo zimeathiriwa na virusi vya Corona zimetoa illani ya usafiri kwa watalii.

Wakuu was sekta ya Utalii katika kaunti ya Samburu wameeleza hofu ya sekta hiyo kusambaratika kabisa. Afisa mkuu wa Utalii katika kaunti ya Samburu Joy Letoiya alisema kuwa hoteli nyingi na vivutio vya watalii vimeshuhudia uhaba wa wageni kwa mwezi mmoja iliyopita.

“Athari zimeonekana hapa Samburu. Vivutio vya watalii vimekosa wateja na kuwndikisha hasara,” alisema Bi Letoiya.

Kaunti ya Samburu ina vivutio vingi vya watalii ikiwemo kile cha Samburu Lodge na Maralal Safari Lodge.

Watalii huzuru kaunti ya Samburu ili kushuhudia utamaduni mbalimbali ikiwemo tohara na ndoa.

Hata hivyo, Waziri wa Utalii Najib Balala alitangaza Alhamisi iliyopita kuwa serikali imetenga takriban shilingi millioni 500 ili kunusuru sekta hiyo muhimu.

Hayo yakijiri, maafisa wa afya katika kaunti hiyo wamewahimiza wakazi kukumbatia Sheria ili kuzuia usambazaji wa virusi vya Corona.

Waziri wa afya katika ya Samburu Stephen Lekupe aliambia Taifa Leo kuwa serikali ya kaunti imetoa mafunzo kwa manesi wote jinsi ya kuwashughulikia waathiriwa wa virusi hivyo iwapo vitazambaa Samburu.

Alisema serikali ya kaunti hiyo imetenga vitanda vinne ili kusaidia katika shughuli hiyo.

“Kwa sasa manesi wote wamefunzwa namna ya kuwashughulikia waathiriwa wa virusi vya Corona. Vituo vya afya ambavyo vimepokea vitanda maalum ni Maralal, Wamba na Baragoi,” alisema Bw Lekupe.

Alitoa wito kwa wakazi kujihathari na wale watakaonesha dalili za virusi hivyo.

You can share this post!

FKF Nairobi Magharibi yapata viongozi wapya

Watu 3 zaidi wameonyesha dalili za corona – Serikali

adminleo