Coronavirus: Mambo ya kutilia maanani
Maambukizi na Vifo
KUFIKIA jana watu zaidi ya 82,000 walikuwa wamethibitishwa kuambukizwa coronavirus ambapo zaidi ya 2,800 walikuwa wamekufa na wapatao 33,000 wamepona.
Nchi zinazoongiza kwa maambukizi kufikia jana ni China (78,000), Korea Kusini (1,500), Italia (470), Japan (189) na Iran (139).
Dalili
Dalili zake zinategemea na hali ya afya ya mgonjwa. Lakini kwa kawaida huanza kwa joto jingi mwilini ikifuatwa na kikohozi kikavu. Baada ya wiki moja inasababisha matatizo ya kupumua.
Madaktari wanasema dalili kama makamasi, kupiga chafya na vidonda vya koo sio kawaida kwa wanaougua maradhi haya.
Kwa wazee na watu walio na maradhi yasiyo na tiba, dalili kama za numonia, uchungu kifuani na kuzimba pamoja na kushindwa kupumua zinajitokeza.
Walio hatarini zaidi
Watu walio na maradhi yasiyo na tiba wamo kwenye hatari zaidi ya kuambukizwa coronavirus na kufariki. Maradhi haya ni pamoja na mkimbio wa damu, matatizo ya moyo, kisukari na matatizo ya kupumua.
Muda wa kujitokeza
Baada ya kuambukizwa, dalili huanza kujitokeza kwa kati ya siku 2 hadi 14. Hata hivyo kumekuwepo na visa vichache ambapo dalili zinaonekana baada ya siku 19 hadi 27.
Hatari ya kufa kulingana na umri
Wazee ndio wamekufa zaidi kutokana na coronavirus.