• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 6:07 PM
Del Monte kuzindua kiwanda  kipya cha matunda karibuni

Del Monte kuzindua kiwanda kipya cha matunda karibuni

Na NDUNGU GACHANE

KAMPUNI ya kutengeneza bidhaa za matunda ya Del Monte Kenya Limited (DMKL) iko mbioni kukamilisha ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa cha Sh580 milioni, kitakachoiwezesha kutengeneza tani 70,000 za matunda kila mwaka.

Kiwanda hicho kipya, kinachojengwa katika shamba kuu la Del Monte, kinatarajiwa kuanza kazi mwezi jana.

Ujenzi wake ni sehemu ya mkakati mkuu wa kampuni hiyo kupanua biashara yake ya utengenezaji na usambazaji matunda ya mananasi pamoja na matunda mengine ikiwemo parachichi, maembe na karakara.

Meneja Mkurugenzi Stergios Gkaliamoutsas asema kiwanda hicho kipya pia kitaimarisha maisha ya wakulima 2,000 wa matunda katika kaunti za Muranga na Kiambu ambako matunda ya Del Monte yatazalishwa, na vile vile kutengeneza ajira 200 mpya.

“Del Monte Kenya inapanga kuchukua matunda kutoka kwa wakulima wa Murang’ a na Kiambu, ambayo yatatengenezwa na kupakiwa katika kiwanda hicho kipya ili kuuzwa katika soko la humu nchini na kimataifa.

“Kiwanda kipya pia kitaimarisha uchumi wa kaunti hizo mbili kwa kutengeneza ajira 200 mpya na nafasi 2,000 za uchumi kwa wakulima 2,000 wa matunda na mboga watakaowasilisha mazao yao kwa Del Monte Kenya,” alieleza Bw Gkaliamoutsas.

Kampuni hiyo iliyoanza kutengeneza bidhaa za matunda freshi mnamo 2010 kwa sasa husafirisha kontena 4,000 za bidhaa za mananasi na maji ya matunda mengine kupitia bandari ya Mombasa kila mwaka.

Inatoa ajira za moja kwa moja kwa wakazi 6,500, nyumba kwa wafanyakazi zaidi ya 2,000 na ajira za ziada 28,000 kupitia kampuni zingine zinazohusiana na Del Monte Kenya.

Bw Gkaliamoutsas alisema kampuni hiyo imeshuhudia ukuaji mkubwa tangu 2010 hususan kupitiaa bidhaa yake mpya ya mananasi ya Del Monte Gold Extra.

Hii imeiletea tuzo kutoka taasisi mbalimbali kama kampuni kubwa ya pekee ya Kenya inayouza mananasi nje ya nchi pamoja na matunda mengine ya tropiki – na kuiletea taifa zaidi ya Sh9 bilioni kila mwaka.

  • Tags

You can share this post!

Demu pabaya kujilipia mahari

Wauzaji vitabu walia wanapata hasara

adminleo