• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Deni la mabilioni lamwandama Biwott kaburini

Deni la mabilioni lamwandama Biwott kaburini

WYCLIFF KIPSANG NA TITUS OMINDE

Mwanasiasa maarufu Nicholas Biwott aliaga dunia miaka miwili iliyopita lakini deni linaendelea kumwandama hadi kaburini. Hii ni baada ya mfanyabiashara mmoja mjini Eldoret kuelekea mahakamani akitaka kulipwa Sh6 bilioni kutoka kwa familia ya marehemu Biwott anazodai alimkopesha kati ya Novemba mwaka wa 2015 na Septemba 2016

Bw Barnabas Kiprono anataka kulipwa Sh382 milioni alizomkopesha marehemu Biwott pamoja na riba ya Sh6 bilioni ambazo kwa jumla ni Sh6.3 bilioni. Kesi hiyo ilifaa kusikizwa jijini Nairobi kwa pamoja na nyingine inayohusu mali ya marehemu lakini Bw Kiprono akapinga kuhamishiwa kwa kesi yake hadi Nairobi akisema kesi hiyo nyingine haihusiani na kesi yake.

Mahakama ilikubali malalamishi ya Bw Kiprono na kesi yake itasikizwa tarehe Oktoba 8 mwaka huu.

Bw Kiprono alikuwa ameelekea mahakamani mnamo Februari 28 mwaka huu akidai deni lake.

Bw Biwott aliaga dunia Julai 11,2017 kutokana na saratani akiwa na miaka 77. Jaji mkuu Olga Sewe alitupilia mbali ombi la watu wa familia ya Biwott waliotaka jina la Kiprono liondolewe katika orodha ya wanaopaswa kufaidika na mali ya mbunge huyo wa zamani wa Keiyo Kusini.

Bw Kiprono anataka mahakama isimamishe kugawa mali ya Bw Biwott hadi kesi hiyo isikizwe.

Baadhi ya mashamba ambayo Bw Kiprono anataka yasigawiwe ni kama vile yenye nambari: 1/809 (Original No 1/37/4), No 27815, No 8125, Eldoret Municipality Block 4/2, Eldoret Municipality Block 7/41 and Kilifi/Jimba/362.

Mengine ni kama vile Chembe/Kibambashe/377, Subdivision 167 Section VI Mainland North, Keiyo/Upper Cheptebo “A”/1, Mosop/Kaptarakwa/ 472 na Mosop 6 (KUTSI) /1.

Bw Kiprono anadai kuwa atapata hasara kubwa mali hiyo ikigawanywa kabla ya kulipwa deni lake.

Hata hivyo, wanaotaka kutekeleza wasia wa Bw Biwott kupitia kwa wakili wao John Wananda wanataka kesi hiyo itupiliwe mbali. Wanadai mahakama haina uwezo wa kuskiza kesi ya Bw Kiprono.

Jaji Sewe hata hivyo amesema kuwa kesi hiyo inahusu pesa nyingi na haiwezitupiliwa mbali.

Alisema mahakama hiyo ina uwezo wa kuskiza kesi ya Bw Kiprono kama mahakama makuu.

Bw Kiprono ametoa mahakama, stakabadhi ikiwemo sahii ya makubaliano alizoandika Bw Biwott ili akopeshewe hela hizo.

You can share this post!

Wakazi wa Thika wapinga ujenzi wa bwawa

Wazazi wa Kyanguli hatimaye wafidiwa Sh53m

adminleo