• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 3:09 PM
Deni la Sh1 bilioni linavyotisha kusamabratisha Ukwala

Deni la Sh1 bilioni linavyotisha kusamabratisha Ukwala

Na BERNARDINE MUTANU

Huenda duka la rejareja la Ukwala likafunga biashara yake kutokana na deni kubwa la takriban Sh1 bilioni ikiwa litaruhusiwa na mahakama.

Duka hilo lilifika mahakamani kutaka kufungwa kabisa kwa biashara yake kutokana na deni hilo.

Duka hilo lina deni la Sh840 milioni la KRA baada ya kushindwa kulipa ushuru. Watoaji 300 wa bidhaa kwa duka hilo pia wanalidai duka hilo mamilioni.

Mwaka jana, duka hilo lilifika mahakamani baada ya kufilisika kutaka kuruhusiwa kumaliza biashara.

Kulingana na malalamishi ya wakopeshaji wake, duka hilo lilikuwa na deni la Sh930 milioni licha ya kuwa mali ya duka hilo ni Sh19.3 milioni.

Mkurugenzi wa duka hilo Vijay Jayantilal Dodhia katika stakabadhi mahakamani alisema kuwa duka hilo lilikuwa limeshindwa kulipa wakopeshaji, wafanyikazi na watoaji wa bidhaa na huduma na kwamba deni lilikuwa kubwa zaidi ya mali yake yote.

Uamuzi kuhusu ombi hilo utatolewa Machi 14. Duka hilo lilifunguliwa 1995 na limekuwa miongoni mwa maduka makubwa zaidi ya rejareja nchini.

  • Tags

You can share this post!

Ebrahims yatia kikomo kwa biashara ya miaka 75

Outering haijapunguza msongamano licha ya kupanuliwa

adminleo