• Nairobi
  • Last Updated May 21st, 2024 3:55 PM
Diwani aliyeuawa alikuwa msitari wa mbele kulaani ujangili

Diwani aliyeuawa alikuwa msitari wa mbele kulaani ujangili

NA GEOFFREY ONDIEKI

PAUL Leshimpiro, Mwakilishi wa Wadi katika Kaunti ya Samburu ambaye aliuawa Jumapili iliyopita, alikuwa akiangazia sana masuala ya usalama katika eneo hilo huku akiomba serikali kuongeza juhudi kukomesha tishio la mashambulizi ya majangili.

Bw Leshimpiro, daktari aliyegeuka kuwa mwanasiasa, wakati mmoja alimuomba Rais William Ruto, kuingilia kati kibinafsi, kukomesha ujangili katika baadhi ya maeneo ya Samburu.

Wadi ya Bw Leshimpiro, Angata Nanyekie, ni mojawapo ya maeneo ambapo majangili wenye silaha wamekuwa wakishambulia wakazi.

Bw Leshimpiro alipigwa risasi Jumapili alasiri, na watu wanaoshukiwa kuwa majangili katika eneo la Soit Pus, kando ya barabara ya Maralal-Baragoi.

Wenyeji katika Kaunti ya Samburu walipigwa na butwaa kufuatia taarifa za kushtusha za kifo cha ghafla cha Bw Leshimpiro, ambaye aliuawa kinyama kwa risasi moja katika kisa cha ujangili.

Bw Leshimpiro, ambaye safari yake kutoka sekta ya matibabu hadi siasa ilivutia wenyeji, alijulikana kwa kujitolea kwake bila kuyumbayumba kutumikia jamii yake kama daktari hata baada ya kuchaguliwa kuwa diwani wa Wadi ya Angata Nanyekie mnamo 2017.

  • Tags

You can share this post!

Mwanamume kulipa faini ya Sh100,000 kwa kuiba mananasi...

Polisi amuua askari jela katika duka la pombe ya makali

T L