• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 8:55 PM
DPP aomba mwezi mmoja zaidi katika kesi ya Cohen

DPP aomba mwezi mmoja zaidi katika kesi ya Cohen

Na RICHARD MUNGUTI

MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) ameomba mahakama kuu apewe muda wa mwezi mmoja kukamilisha zoezi la kumpa ushahidi Sarah Wairimu Kamotho katika kesi inayomkabili ya kumuua mumewe , Tob Cohen.

Bw Cohen, alikuwa mwekezaji bilionea kutoka Uholanzi aliyetoweka Julai 2019 na maiti yake ikapatikana ndani ya tangu nyumbani kwake mtaani Kitisuru Nairobi.

Naibu wa DPP Alexander Muteti alimweleza jaji Jessie Lesiit kuwa “kuna ushahidi ambao haujakamilishwa kuunganishwa ndipo Sarah na wakili wake Philip Murgor wakabidhiwe.”

Bw Muteti aliomba mahakama iruhusu upande wa mashtaka kipingi cha mwezi mmoja ukamilishe kuandaa ushahidi huo na kuwakabidhi washtakiwa Sarah na Peter Karanja ambao wamekana kumuua Cohen na kutupa maiti yake ndani ya tangi la maji.

Polisi waliutafuta mwili wa marehemu kwa zaidi ya miezi miwili.

“Naomba mahakama iwakubalie maafisa wa polisi kukamilisha kuweka pamoja nakala za ushahidi ndio wawakabidhi washtakikiwa katika muda wa mwezi mmoja,” alisema Bw Muteti.

Lakini ombi hilo lilipingwa na wakili Philip Murgor akisema, “sasa ni siku 145 tangu Sarah akamatwe na kuzuiliwa kwa mauaji ya mumewe.”

Wakili huyo alisema maafisa wa upelelezi wamechukulia suala hili la kuandaa ushahidi kama mzaha.

Bw Murgor alisema kwa vile Jaji Stellah Mutuku hakuwa kazini aliomba kesi hiyo itajwe mbele yake ndipo atoe maagizo barabara kulingana na jinsi alikuwa ameamuru DPP amkabidhi Sarah ushahidi wote “kufikia Januari 27 2020.”

Kesi dhidi ya Sarah na Karanja itaanza kusikizwa Julai 2020.

Wawili hao wamekanusha walimuua Cohen. Wako nje kwa dhamana ya Sh2 milioni pesa tasilimu kila mmoja.

Jaji Lesiit aliamuru kesi hiyo itajwe Machi 3, 2020 kwa maagizo zaidi kuhusu nakala za mashahidi.

You can share this post!

Uhuru aadhibu wasiofuata nyayo zake

Gavana Nyoro huru kuteua naibu wake

adminleo