Habari Mseto

Drama Abenny Jachinga akizikwa

June 12th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA RUSHDIE OUDIA

Kulishuudiwa mvutano kati ya wananchi na polisi eneo la Chinga kaunti ya Kisumu wakati mwili wa mwimbaji Bernard Onyango Obonyo, anayejulikana kama Abenny Jachinga ulipelekwa kuzikwa Mowlem Ijumaa asubuhi.

Polisi walikuwa na wakati mgumu kuwathibiti mamia ya waombolezaji waliojiunga na msafara uliosafirisha mwili wa msanii huyo kutoka chumba cha kuhifadhi maiti cha Port Florence.

Msafara huo ulilazimika kutumia barabara ya Obote ili kuhepa kupita katikati ya jiji na Kondele. Kutoka Mowlem, msafara huo uliekea kwenye barabara ya Rabour -Chinga iliyoelekea Kadiju ambapo mwendazake atazikwa.

Waombolezaji hao waliotembea mguu kwa kilomita zaidi ya 20 .Nyumbani kwa mwendazake kulikuwa na polisi .

Mashambiki wa mwendazake walitembea chumba cha kuhifadhi maiti cha Kisumu Port Florence kuona mwili wake. Hisia zilikuwa njuu huku mashambiki wakikimbia,kuendesha baskeli na magari ili kuuna mwili wa mwenda zake na kumpa heshima za mwisho.

Polisi walilazimika kutumia vitoa machonzi ili kuwatanya mamia ya waombolezaji waliokuwa wakiomba mwili wa mwenda zake kufanyika upasuaji na kupewa wakati wamuomboleze vizuri.

Polisi walilazimika kuondoka mahala pale baada ya umati wa watu kutoa mwili wa marehemu kutoka kaburi ambapo polisi walikuwa wameiteremsha saduku hio tayari kumzika marehemu.Baada ya kutoa geneza hilo kwenye kaburi walirudisha mwili huo kwenye kchumba cha kuhifadhi maiti cha karibu.

Walikiuka sheria ya kutotangamana.