• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:20 PM
Elachi ajifungia ofisini kuepuka balaa

Elachi ajifungia ofisini kuepuka balaa

 

FAUSTINE NGILA NA COLLINS OMULO

Kulishuhudiwa kizaazaa Jumanne asubuhi kwenye Bunge la Kaunti ya Nairobi wakati madiwani walijaribu kumpa spika wa mbunge hiyo  Beatrice Elachi notisi ya kumtoa mamlakani. Stakabathi hizo zilikuwa zimetiwa sahihi na madiwani 59.

Walikuwa wanataka kumpa amri ya korti ya kutupilia mbali kumteua Edward Gichana kama karani wa bunge.

Bi Elachi alijifungia kwa afisi yake huku polisi wakizuia madiwani kuingia kwenye ofisi hio.

Waliwatupia vitoa machozi madiwani hao pamoja na wanhabari kwenye majengo hayo .Vita hio ya madiwani na polisi ilimwacha diwani wa Mlango Kubwa Patricia Mutheu na maumivu.

  • Tags

You can share this post!

Beatrice Chepkoech aidhinishwa kutifua kivumbi cha Diamond...

ULIMBWENDE: Jinsi unavyoweza kuchagua manukato yanayokufaa