• Nairobi
  • Last Updated May 8th, 2024 8:55 PM
Faini ya Sh70,000 kwa kusababisha ajali

Faini ya Sh70,000 kwa kusababisha ajali

Na Richard Munguti.

Mwendeshaji bodaboda alitozwa faini ya Sh70,000 kwa kuiendesha upande mbaya wa barabara na kusababisha ajali iliyopelekea abiria wake kupata majeraha ya kudumu.

John Mankura Sintie alikiri mashtaka matatu mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Kibera Nairobi Bw Abdulkadir Lorot.

Hakimu alifahamishwa na kiongozi wa mashtaka George Obiri kwamba mnamo Mei 23 2020 mshtakiwa alikodiwa na Bw Saul Kibeu Nabwela ampeleke karibu uwanja wa Nyayo aabiri matatu.

Mshtakiwa alipitia upamde mbaya wa barabara na kugonga gari iliyokuwa inaendeshwa na James Chege.

Nabwela alijeruhiwa na kupelekwa hospitali..

Akipitisha hukumu Bw Lorot alisena mshtakiwa alihatarisha maisha ya wengi kwa kuendesha piki piki upande usio ruhusiwa kisheria.

“Watu wengi nchini wamepoteza maisha yao katika mikono ya madereva wa magari na boda boda wasiojali,” alisema hakimu.

Bw Lorot aliendelea na kumweleza mshtakiwa kwamba anastahili adhabu kali.

“Ili iwe funzo kwa madereva wengine wasiozingatia sheria kama wewe utalipa faini ya Sh70000 ama utumikie kifungo cha mwaka mmoja gerezani,” hakimu alimuhukumu mshtakiwa.

Pia alifutilia mbali leseni ya mshtakiwa kwa kipindi cha miaka mitatu..

Alipewa siku 14 kukata rufaa.

  • Tags

You can share this post!

Hasara kwa wakulima mboga zao zikikosa soko

Mwanawe Kajembe azikwa