• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 4:54 PM
Familia ya mwanajeshi yataka mwili wa mkewe ufukuliwe

Familia ya mwanajeshi yataka mwili wa mkewe ufukuliwe

Na JOSEPH OPENDA

FAMILIA ya afisa wa Jeshi la Kenya (KDF) ambaye alifariki kwenye shambulio la kundi la kigaidi la Al-Shabaab lililotokea El Adde, Somalia, inataka mwili wa mke wake ufukuliwe.

Familia hiyo inadai mwili wa Bi Esther Muthoni ambaye alikuwa mke wa marehemu Kapteni Joseph Mbau Gichuhi, ulizikwa kisiri alfajiri bila wao kujua.

Bi Muthoni alifariki kwenye ajali iliyotokea Kikopey, katika barabara kuu ya Nakuru-Nairobi wiki mbili zilizopita.

Mwili wake ulizikwa na jamaa zake Jumanne saa kumi na mbili alfajiri.

Mazishi yake yalifanyika kwenye kipande cha ardhi kilichotengwa katika eneo la Kongasis, Kaunti Ndogo ya Gilgil, Kaunti ya Nakuru. Wakazi wa eneo hilo walitazama kwa umbali wakistaajabishwa na hali hiyo isiyo ya kawaida.

Familia ya marehemu mume wake ilisema walikuwa wamepata agizo la mahakama kuzuia mazishi yake lakini wakashangaa walipoambiwa mwili ulikuwa tayari ushatolewa katika hifadhi ya maiti kuenda kuzikwa.

“Tuliwasili katika mochari mwendo wa saa tatu asubuhi kuwasilisha agizo la mahakama lakini tukashtuka kupata mwili ulikuwa umechukuliwa na familia yake saa kumi na moja alfajiri,” akasema Bw Maina, ambaye ni kakaye mwanajeshi marehemu.

Bw Maina alisema familia yake iliamua kuenda mahakamani baada ya familia hizo kushindwa kukubaliana kuhusu mahali pa kuzika mwili wake.

  • Tags

You can share this post!

Agizo la Rais laletea kiwanda cha nguo Kitui sifa kubwa

Serikali yashirikisha viongozi wa dini kukabiliana na ugaidi

adminleo