• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Fujo tele #SabaSaba

Fujo tele #SabaSaba

Na MARY WAMBUI

WAANDAMANAJI kadhaa waliokuwa wakiadhimisha siku ya Saba Saba jijini Nairobi jana walikamatwa, na maandamano yao kuvurugwa na polisi waliowarushia vitoa machozi.

Wakili John Khaminwa, na wanaharakati George Kegoro na Florence Kanyua walitaka waandamanaji waliokamatwa waachiliwe katika Kituo cha Polisi cha Kilimani. Walisema ijapokuwa polisi walikataa maandamano yasifanywe, maandamano yamelindwa kikatiba na ilikuwa jukumu la polisi kutoa ulinzi.

Kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi katikati ya jiji, ambao walikimbizana na waandamanaji walioendelea kutokea kila wakati wakitawanywa.

Maadhimisho hayo ya 30 ya Saba Saba, ambayo huadhimisha siku ambapo maandamano ya kitaifa yalifanyika 1990 kupigania siasa ya vyama vingi, mwaka huu yalisheheni wito wa kutetea haki za binadamu.

Miongoni mwa masuala ambayo waandamanaji walitetea ni hitaji la polisi kukoma kuangamiza raia kiholela.

You can share this post!

Changamoto kuzuia wazee katika ibada

Mlima Kenya tunalenga minofu 2022 – Murathe

adminleo