• Nairobi
  • Last Updated April 30th, 2024 5:46 PM
Gavana Mutua apongeza hatua za kudhibiti corona

Gavana Mutua apongeza hatua za kudhibiti corona

NA LILLIAN MUTAVI

Gavana wa Machakos Alfred Mutua amepongeza kuongezwa kwa siku za kafyu na makataa ya kutotoka au kuingia Nairobi, Mombasa na Mandera akisema kwamba kuongezeka kwa visa vya corona kunahitaji tahathari hizo.

Akiongea Jumatatu alisema kwamba visa vya corona vilivyoshuhudiwa Machakos vimetokea Nairobi kutokana na madereva wa kusafirisha mizigo wanaopitia Machakos kutoka Mombasa.

Gavana huyo alisema kwamba anaunga mkono Rais Uhuru Kenyatta kwa kuweka mikakati aliyoweka ili kukabiliana na corona.

Alisema kwamba Machakos wametenga vitanda 350 na ambulensi 9 kila kaunti ndogo ili kupambana na virusi vya corona.

“Tukona bahati sana kwa sababu tuko na maabara ya kupima corona na tumeagiza vitanda vingine.”

Ili kuzuia madereva wa maroli kutangamana na wananchi wengine, malori yanaruhusiwa kusimama kujaza mafuta pekee Machakos.

You can share this post!

Chifu anaswa akimumunya hongo

Wanariadha waliosafiri India warudi humu nchini

adminleo