Hali ngumu ya uchumi yashusha uzalishaji wa saruji
Na BERNARDINE MUTANU
UZALISHAJI wa saruji ulishuka kwa kiwango kikubwa 2017.
Hiyo ilikuwa ishara ya kushuka kwa viwango vya ujenzi wa majumba na mitaa nchini.
Hali hiyo inaaminika kutokna na hali ngumu ya uchumi nchini.
Uzalishaji wa simiti ulishuka kwa asilimia 8.2 (tani 550,000) kufikia Desemba 2017.
Kulingana na takwimu kutoka shirika la takwimu nchini (KNBS) katika kipindi hicho, tani 6.16 milioni zilizalishwa.
Kiwango cha juu zaidi kilizalishwa Machi, ambapo tani 570,522 zilizalishwa ambapo kiwango cha chini ilikuwa ni Mei, ambapo tani 482,762 zilitengenezwa.
Matumizi ya simiti yalipungua kwa asilimia 8.12 hadi tani 6.30 milioni, ishara kwamba hakukuwa na shughuli nyingi katika sekta hiyo.