Habari Mseto

Hali ngumu zaidi baada ya bei ya mafuta kupanda tena

April 14th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na VALENTINE OBARA

WAKENYA watazidi kukumbwa na hali ngumu ya maisha na hata kulemewa zaidi baada ya bei ya mafuta kuongezeka kwa kiasi kikubwa.

Tume ya Kudhibiti Kawi (ERC) Jumapili ilitangaza ongezeko la bei ya mafuta wakati ambapo bidhaa nyingine muhimu pia zinazidi kupanda bei.

Kwenye tangazo kuhusu bei mpya za mafuta ambayo itatumika hadi mwezi ujao, bei ya mafuta taa itapanda kwa Sh2.76 huku ile ya Diesel ikipanda wka Sh5.52 na Super Petrol ikiongezeka kwa Sh5.25.

ERC ilisema ongezeko hilo limetokana na jinsi bei ya mafuta inayoagizwa kutoka nchi za kigeni ilivyopanda.

Jijini Nairobi, mafuta ya Super Petrol itakuwa Sh106.6 kwa lita moja, Diesel Sh102.13 na mafuta taa Sh102.22. Mafuta ya Super Petrol Mombasa yatauzwa kwa Sh103.98 kwa lita moja, Diesel Sh99.51 na mafuta taa Sh99.60.

Mkurugenzi Mkuu wa ERC, Bw Pavel Oimeke alisema tume yake imejitolea kuhakikisha maslahi ya wateja yanalindwa