• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 6:55 PM
Hija yaanza rasmi

Hija yaanza rasmi

Na FARHIYA HUSSEIN

Waislamu nchini wataungana na wengine ulimwenguni kote kuashiria leo kama siku ya kwanza ya sherehe za Hija, Kadhi Mkuu wa Kenya, Sheikh Ahmed Muhdhar amethibitisha.

Maadhimisho hayo yanajulikana kama ‘Hajj’ kawaida hufanywa katika Mji wa Mecca nchini Saudi Arabia.

Walakini mwaka huu, wakenya wakiwemo baadhi ya nchi zinginezo watalazimika kufuata miongozo iliyowekwa ili kuepusha kuenea kwa kirusi cha korona na kuandaa sherehe hizo majumbani kwao.

Hii ni baada ya Saudi Arabia kupiga marufuku wasafiri kutoka nje ya Nchi hiyo kutembelea mji mtakatifu.

“Hapo awali, hatukuona mwezi wowote nchini Kenya. Lakini tumepokea uthibitisho kutoka kwa ndugu zetu wa nchi ya Zanzibar na leo unaashiria siku ya kwanza ya mwezi wa Dhul Hijja, “alisema Sheikh Muhdhar.

Dhul Hijja, ambao ni mwezi wa kumi na mbili na wa mwisho katika kalenda ya Kiislam huonekana kwa wengi kama nafasi ya kuimarisha imani yao.

Mwaka huu, watu 160 pekee kutoka nchi tofauti ambao wanaishi ndani ya Saudia ndio watakaopata nafasi ya kufanya ibada ya Hija.

Kwa wale ambao wamekosa fursa hiyo, wanaweza kuendesha sherehe kupitia njia zinginezo ya kidini.

“Mtu akishindwa kusafiri kwenda Makka kwa ibada ya Hija, anaweza kufunga siku kumi za kwanza za mwezi,kutembelea wagonjwa, kutoa sadaka,” aliongezea Sheikh Muhdhar.

Ibada hiyo hufanyika siku kumi za kwanza za mwezi ambayo yanafuatana na sherehe ya Iid ul Adha.

“Kufuatia kalenda hiyo, tumeanza rasmi sherehe hizo siku ya leo ikiwa Jumatano Julai 22, 2020, kwa hivyo maadhimisho ya Iid Ul Adha yatakuwa Ijumaa Julai 31, 2020,” Kadhi Mkuu alisema.

Aliwasihi Waislamu kutekeleza sala zao na kuhakikisha kwamba wanafuata sharia zilizotengwa ili kupunguza kuenea kwa kirusi cha korona.

You can share this post!

Joho awindwa na EACC

Arsenal yanyongwa na Villa

adminleo