• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Hofu nyumba kumi zikibomolewa Isiolo

Hofu nyumba kumi zikibomolewa Isiolo

NA WAWERU WAIRIMU

Hofu imetanda kwenye Kijiji cha Golan, Kaunti ya Isiolo baada ya kundi la vijana kubomoa nyumba kumi kufuatia mzozo wa ardhi.

Kundi la vijana ambalo lilikuwa limejihami kwa silaha walivamia eneo lililokuwa linaishi wanawake zaidi ya 50 na kubomoa nyumba za mbao ambazo zilikuwa zinaendelea kujengwa huku wakazi wakilazimika kukimbia kujificha.

Huku walioathirika wakikimbilia uhai wao na kujificha Kijiji jirani cha Bulapesa, wavamizi hao waliendelea kubomoa na kutoroka na bidhaa za mamia ya maelfu.

Bi Jane Ntinyari mmoja wa wathiriwa alikuwa akifanya kazi za nyumbani wakati aliwaona vijana hao wakikaribia hapo ndipo alikimbia kuokoa maisha yake.

“Walikuwa wamebeba panga na rungu huku wakitutishia kutuua. Nilijulisha waliokuwa ndani ya nyumbana tukakimbia ili kuokoa maisha yetu,”alisema Bi Ntinyari.

Bi Naima Mohammed alilalamikia  mashambulizi ya kila saa na vikundi vya vijana vilivyolipwa huku akisema kwamba mavamizi hayo yanarudisha maendeleo nyuma.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA

  • Tags

You can share this post!

Vijana waandamana kumkomesha Ruto kutusi Matiang’i

LISHE: Keki ya vanilla isiyo na mayai