• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 8:55 AM
Hofu ya mgawanyiko EAC, kikao kikiahirishwa tena

Hofu ya mgawanyiko EAC, kikao kikiahirishwa tena

Na ZEPHAIA UBWANI

DALILI za kupanuka kwa tofauti kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ziliibuka jana baada ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi hizo kuahirishwa kwa mara ya pili katika muda wa majuma matatu.

Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika katika Jumba la Mikutano ya Kimataifa la Arusha (AICC) mnamo Desemba 27, ila umeahirishwa hadi itakapotangazwa tena.

“Ni rasmi. Mkutano huo hautafanyika mnamo Desemba 27 kama ilivyopangwa,” akasema Naibu Katibu Mkuu wa jumuia hiyo Christophe Bazivamo.

Aliiambia gazeti la ‘The Citizen’ kwamba tarehe na mahali papya ambapo mkutano huo utafanyika patatajwa baadaye ambapo mataifa yote wanachama yatafahamishwa.

Na kando na kuahirishwa kwa mkutano huo, kikao cha mawaziri wa.. ambacho kilipangiwa kuanza jana pia kilifutiliwa mbali ghafla katika dakika za mwisho.

Duru zilieleza kwamba huenda mkutano huo ukaandaliwa muda wowote kuanzia mwezi Februari au Machi mwaka ujao.

Hilo linatarajiwa kuwapa waandalizi muda wa kutosha kutathmini kwa kina mustakabali wa jumuiya hiyo, hasa kutokana na tofauti za kindani miongoni mwa baadhi ya wanachama wake.

Hata hivyo, Bw Bazivamo hakueleza sababu za zilizosababisha mkutano huo kuahirishwa tena, baada ya wa kwanza kutofanyika mnamo Novemba 30 baada ya Burundi kusema haingeshiriki.

“Marais wa nchi wanachama wangali wanaendelea kushauriana kuhusu suala hilo,” akasema, bila kutoa ufafanuzi zaidi.

Katibu huyo ndiye alikuwa afisa wa kwanza wa ngazi za juu wa jumuiya hiyo kufichua kwamba kuna tofauti zilizosababisha kutofanyika kwake.

Mnamo Jumanne, alieleza kuwa huenda mkutano huo ukakosa kuandaliwa.

Kufikia jana jioni, Kitengo cha Mawasiliano katika jumuiya hiyo hakikuwa kimetoa taarifa yoyote rasmi kuhusiana na hatua hiyo.

Wachanganuzi wa masuala ya kikanda walisema kwamba hawakushangazwa na hatua hiyo, hasa baada ya majibizano m

You can share this post!

Makachero wanasa polisi wanne waliopora mfanyabiashara fedha

Kericho, Bomet kufikishwa kortini kwa kuhudumu bila...

adminleo