• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Hospitali ya Aga Khan kuwafanyia uchunguzi wa bure wanaohitaji upasuaji wa urekebishaji

Hospitali ya Aga Khan kuwafanyia uchunguzi wa bure wanaohitaji upasuaji wa urekebishaji

Na WACHIRA MWANGI na FARHIYA HUSSEIN

HOSPITALI kuu ya Aga Khan pamoja na shirika la kimataifa la kuwasaidia wanawake la Reconstructing Women International, watawafanyia uchunguzi wa bure wanawake na wasichana wanaohitaji upasuaji Ijumaa.

Daktari msimamizi wa hospitali hiyo, Dkt Sultana Sherman amesema mradi huo utawasaidia wanawake na watoto wa kike ambao wamepata changamoto mwilini baada ya kuchomeka.

“Mpango huu unanuia kuwasaidia wanawake waliochomeka ama kwa sababu ya ajali ya moto, kunyanyaswa nyumbani na kuishia kupata ulemavu kutokana na hayo,” akasema Dkt Sherman.

Alisema kuwa mara nyingi wauguzi hao hawana nguvu kwenye sehemu walizochomeka kimwili na ndiyo maana upasuaji huo wa bure utawasaidia kupata afueni kidogo.

Wale ambao watanufaika watajiandaa kwa matibabu ya bure mwezi wa Agosti.

Daktari huyo alisema kuwa wanawake na wasichana nchi tofauti wanahitaji upasuaji huo lakini wanakosa madaktari au wataalamu wa upasuaji wa kuwashughulikia.

“Akina mama zetu huwa katika kiwango cha juu cha hatari ya moto wanapopika na ndiyo maana ni muhimu kuwapa upasuaji huu kuwaonyesha heshima na umuhimu wao katika jamii,” akasema Dkt Sherman.

Alisema kuwa mwaka 2018 walishughulikia wagonjwa 99 na miongoni mwao, 30 walifaidika kutokana na upasuaji huo.

Wanatarajia mwaka huu idadi itaongezeka hadi 50.

Timu hiyo ya upasuaji inafanya kazi nchi kama India, Bangladesh, Pakistan, maeneo ya Afrika Mashariki na Haiti.

Aidha, Dkt Sherman alisema kuwa kwa kawaida gharama ya kumshughulikia mgonjwa mmoja ni Sh300,000.

  • Tags

You can share this post!

Posta Rangers yalaza Nairobi Stima na kusalia katika ligi...

Baraza la Agikuyu sasa lamtaka Rais atangaze msimamo wake...

adminleo