Hoteli zaomba saa za huduma ziongezwe
NA BONFACE OTIENO
Hoteli na maeneo ya burudani yanaiomba serikali kuongeza wakati wao wa kufanya kazi ili waongeze mapato yao huku sekta hiyo ikikumbwa na hasara kuu kutokana na virusi vya corona vilivozua kupungua kwa wateja.
Mwenyekiti wa chama cha mahoteli, vilabu na maeneo ya burudani alisema kwamba hoteli zinafaa zifanye kazi kunzia saa kumi na moja asubuhi mpaka saa mbili usiku, kikiongezea kwamba saa chache zinawanyima biashara.
“Tunaiomba serikali ituongezee saa za kufanya kazi kuanzia saaa kumi na moja asubuhi hadi saa mbili jioni. Wateja wetu hututembelea baada ya kazi hivyo kufunga kwetu saa kumi inakuwa ngumu,” alisema Bi Opee.
Serikali iliziruhusu hoteli zilizokuwa zimesimamisha kazi kwa sababu ya corona kurudi kazini na zifanye kazi kuanzia saa kumi na moja asubuhi hadi saa kumi jioni.
Serikali jana ilishikilia hoteli na mikahawa zinafaa kufuatilia mikakati mpya iliyowekwa .
Bi Opee alisema kwamba serikali iliongeza saa za kafyu kuanzia saa tatu usiku usiku mpaka saa kumi asubuhi.