• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 3:24 PM
Jaji Odek alifariki kwa damu kuganda mguuni – Serikali

Jaji Odek alifariki kwa damu kuganda mguuni – Serikali

Na VICTOR RABALLA

RIPOTI ya upasuaji imeonyesha kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Otieno Odek alifariki baada ya damu kuganda kwenye mguu wake wa kulia.

Kulingana na Mpasuaji Mkuu wa serikali Johansen Oduor, kuganda kwa damu mguuni kulisababisha damu kushindwa kufika katika mapafu.

“Kutokana na hilo, moyo uliishiwa nguvu na kumfanya Jaji Odek kufariki kimya kimya,” Dkt Oduor akaambia wanahabari jana baada ya kukamilisha shughuli ya upasuaji katika Hospitali ya Aga Khan, Kisumu.

Dkt Oduor pia alipuuzilia mbali madai kwamba huenda jaji huyo alifariki baada ya kumeza tembe.

Jaji Odek alipatikana ameaga dunia katika nyumba yake ya kupanga ndani ya jumba la Groove Hut Apartment jijini Kisumu mnamo Desemba 16.

Dkt Oduor alisema kuwa hali ya mwili wa Jaji Odek, 56, inaonyesha kwamba alifariki kati ya Jumamosi Desemba 14 au Desemba 15.

“Alifariki kati ya siku mbili na tatu kabla ya mwili wake kugunduliwa,” akasema Dkt Oduor alipokuwa akihutubia familia ya mwendazake huku akiwa ameandamana na Afisa Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu (DCI) wa Kaunti ya Kisumu Arap Towett pamoja na Mpasuaji Mkuu wa Serikali wa ukanda wa Magharibi Dkt Dixon Mchana.

Dkt Oduor alikuwa katika hatari ya kufariki kutokana na ugonjwa wa ‘Pulmonary Thrombo-Embolism’ ambao hutokana na kuketi kwa muda mrefu.

Alisema kuwa ripoti hiyo itakabidhiwa idara ya DCI kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Shughuli ya upasuaji ilifaa kufanyika Alhamisi lakini ikaahirishwa kutokana na agizo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa DCI George Kinoti.

  • Tags

You can share this post!

KRISMASI: Ni wakati wa kupunguza siasa, viongozi waambiwa

2019: Sonko alivyotumia majina 5 kufanikisha ufisadi

adminleo