• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
Jamii ya Kalenji yamwomboleza msanii Kaboom

Jamii ya Kalenji yamwomboleza msanii Kaboom

NA PHYLLIS MUSASIA

Jamaa na marafiki wa aliyekuwa mwanamuziki wa jamii ya Kalenjin Harmon Kipkurui Rono wamemwomboleza mpendwa wao.

Rono, ambaye alijulikana kama Kaboom alifariki kwenye ajali ya barabara kwenye barabara ya Emining-Eldama Ravine.

Alikuwa na miaka 26 na alifariki saa moja na nusu jioni alipokuwa akielekea Eldama Ravine akitoka soko la Mogotio ambapo alikuwa afanye mkutano na mashambiki wake.

Familia ilisema kwamba pikipiki ya Rono iligongwa na gari lililokuwalimeendeshwa kwa kasi.

Familia pia ilikana madai kwamba Bw Rono alikuwa mlevi wakati ajali ilipotokea. Familia na marafiki walimtaja Kaboom kuwa mtu mwenye kujiamini.

Binamuye Victor Cheruiyot alitaja mwanamziki huyo kuwa mtu mnyenyekevu, mchapakazi na aliyekuwa anajua wajibu wake na mwenyekujitolea.

“Aliishi Eldama Ravine kwasababu alikuwa anafanya kazikwa studio mji huo lakini roho yake ilikuwa nyumbani kwani yeye ndiye alishungulikia familia yao baada ya babayake kufariki 2001,’ alisema Bw Cheruiyot.

Mjombawake  Robert Kimutai,alisema kwamba Robert  Kimutai alisema kwamba Bw Rono hakuwa amelewa kama ilivyosemekana.

“Niliona akikua tangu babayake afariki na amekuwa mtu mzuri ,” alisema. Kaboom ambaye alizaliwa Londiani,kaunti ya Kericho na yeye ndiye kifungua mimba wa familia ya watoto watano.  Aliishi na mkewe wa miaka 23 na mwana wao wa miaka mitatu.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA

 

  • Tags

You can share this post!

Waliniombea nife nilipougua corona – Gavana

Milioni 1.5 wameambukizwa corona Afrika – kituo...