Habari Mseto

Jela maisha kwa kubaka mtoto

July 5th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

CHARLES WANYORO na FAUSTINE NGILA

Mwanume aliyembaka msichana wa miaka mitano kaunti ya Meru ametupwa ndani maisha.

Hakimu Millicent Nyigei alisema upande wa mashtaka ulitoa ushaidi wa kutosha kwamba David Mwenda wa miaka 30 alidanganya mtoto huyo na kumdhulumu kimapenzi alipokuwa akicheza na wenzake Igembe Kusini.

Katika kusikizwa kwa kesi miezi tisa iliyopita, upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi watano wakiwemo watoto wawili ambao wanalimtambua mshukiwa huyo.

Alimdanganya msichana huyo na kumuingiza kwenye chumba kilichokuwa kikijengwa, hapo ndipo alimtoa nguo na akambaka.

Alipiga ukemi kwa uchungu lakini mwanaume huyo akamfunika mdomo kwa koti. Lakini kuna kijana mmoja alisikia kilio hicho na akaenda kuchunguza nini kilikuwa kinaendelea na kumfumania.