• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Jowie azidi kupambana kubatilisha hukumu ya kifo

Jowie azidi kupambana kubatilisha hukumu ya kifo

Na BRIAN OCHARO

JOSEPH Kuria Irungu almaarufu Jowie, aliyehukumiwa kifo kwa mauaji ya mfanyabiashara Monicah Kimani jijini Nairobi, ameanzisha juhudi nyingine za kisheria kusaka uhuru kwa kupinga uhalali wa hukumu ya kifo katika kesi ambapo watu wanashtakiwa na kuhukumiwa kwa mauaji.

Hizi ni juhudi za pili za kisheria ambazo Jowie ameanzisha dhidi ya serikali ili pate uhuru wa mapema baada ya nyingine anayotaka hukumu ya kifo aliyopewa mwezi uliopita na Mahakama Kuu ibatilishwe.

Jowie amerejea katika Mahakama Kuu kupitia ombi la kikatiba ambapo anataka kufutiliwa mbali kwa Kifungu cha 379(4) cha Sheria kinachotoa hukumu ya kifo, akisema ni kinyume cha Katiba kwa kuwa kinawanyima watu waliohukumiwa kifo haki ya kupewa dhamana wanaposubiri rufaa.

Jowie anadai kuwa kifungu hicho cha sheria kinabagua na kukiuka haki ya binadamu ya mtu aliyehukumiwa kunyongwa na hivyo kwenda kinyume na ibara ya 27 na 28 ya Katiba.

“Mlalamishi anaomba iamuliwe kwamba adhabu ya kifo katika asili yake, na kwa namna, mchakato na namna inavyoweza kutekelezwa ni mateso, ukatili, unyama na ya udhalilishaji iliyopigwa marufuku chini ya Ibara ya 25 ya Katiba,” alisema Jowie.

Pia, Jowie anahoji kuwa hukumu ya kifo aliyopewa kwa mauaji ya mwanamke mfanyabiashara Monica Kimani ilikiuka haki yake ya kuishi iliyolindwa chini ya Kifungu cha 26(1) cha Katiba.

Pia, anataka iamuliwe kwamba sheria nyingine zote zinazotoa hukumu ya kifo nchini Kenya zinakiuka Vifungu vya 25 na 26 vya Katiba kwa kiwango ambacho zinaruhusu au kuagiza kutolewa kwa hukumu za kifo.

“Mlalamishi anaomba iamuliwe kwamba hukumu ya kifo Machi 13, 2024 inakiuka haki yangu ya uhuru kulindwa, mateso na ukatili, unyama au udhalilishaji au adhabu,” Jowie alisema.

Jowie alihukumiwa Machi 13, mwaka huu kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua Bi Kimani katika mtaa wa Limuria Garden, jijini Nairobi.

Jaji Grace Nzioka, baada ya kuchambua ushahidi katika kesi hiyo, aligundua kuwa mfungwa huyo alimuua Monicah Kimani na akaamua kuwa alistahili hukumu ya kifo.

Jaji alibainisha kuwa mfungwa alimuua Bi Kimani na kumwacha amefungwa ndani ya bafu.

Ushahidi kama vile kuteketezwa kwa Kanzu ambayo mfungwa huyo alikuwa amevalia ulikuwa ni kujaribu kuficha ushahidi.

Mahakama pia ilitegemea ushahidi wa upande wa mashtaka kwamba marehemu hakumchokoza mfungwa kiasi cha kumshambulia na kusababisha kifo chake.

  • Tags

You can share this post!

Mvuvi aliyefariki akisubiria fidia ya Lapsset

Upinzani umelala tangu Raila aanze kuwania kiti AU

T L