• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 8:50 AM
Kamishna azuru kijiji cha Kisii Thika kuzima mzozo unaohusu vipande vya ardhi

Kamishna azuru kijiji cha Kisii Thika kuzima mzozo unaohusu vipande vya ardhi

Na LAWRENCE ONGARO

WALAGHAI wa vipande vya ardhi katika Thika Magharibi wameonywa kuwa siku zao zimewadia.

Naibu kamishna wa eneo hilo Bw Douglas Mutai alisema tayari wamepokea majina ya wale wote wananaoshukiwa kuwa ni walaghai wa vipande vya ardhi huku akisema anaendelea na uchgunguzi.

Mnamo Ijumaa Bw Mutai alizuru kijiji cha Kisii, mjini Thika, eneo ambalo limekuwa na utata kuhusu maswala ya umiliki wa vipande vya ardhi.

Wiki moja iliyopita familia zaidi ya 20 zilifurushwa kutoka katika makazi zao walikojenga wakielezwa kuwa eneo hilo lina wenyewe.

Bw Mutai ambaye alifika mahali hapo kutatua malalamishi yao aliwahakikishia wakazi hao kuwa kutoka wakati huo hawata hangaishwa na yeyote tena.

“Ninaelewa kuna kampuni moja ya kuuza vipande vya ardhi iliyoko eneo la Kilimambogo lakini washukiwa wote wanajulikana. Hakuna yeyote aliye na haki ya kubomoa mali ya mwingine. Iwapo una shinda na mwenzako kuna sheria neda uripoti jambo linalokukera,” alisema Bw Mutai.

Aliwaamuru wale wote wanaodai kuwa ndio wenye shamba hilo la Kisii wafike kwa afisi yake mara moja na stakabadhi zinazohitajika vya umiliki wa shamba hilo.

“Iwapo una stakabadhi zako muhimu kuja navya katika afisi yangu ili twende wizara ya ardhi na kuthibitisha hayo. Ni lazima tukomeshe wale wote wanaotaka kuibia watu mali zao,” alisema Bw Mutai.

Bw Irungu Kuria, mkazi wa eneo hilo anasema alinunua ploti mahali hapo mwaka wa 2013 na kujenga makazi yake hapo.

“Tunaiomba serikali kufanya hima kuona ya kwamba wale matapeli wanaohangaisha wakazi wa hapo wanachukuliwa hatua ya kisheria,” alisema Bw Kuria.

Bi Joyce Wanjiku anasema ameishi katika mahali hapo kwa zaidi ya miaka mitano na inashangaza kuona ya kwamba mtu anaweza kuja vipi kusema mahali fulani ni kwake na hata hajaona stakabadhi zako ?

Hivi majuzi wahuni waliojihama kwa vifaa butu walifika katika kijiji hicho na kuanza kuwafurusha wakazi hao .

Wakati wa kitendo hicho wakazi wengi walitoroka kutoka makazi zao kwa kuhofia maisha yao kwani

Naibu kamishna huyo aliwataka wakazi walioathirika kutokana na ubomoaji huo wajihami na vyeti vyao vya umiliki katika afisi yake ili baadaye wakafanye uchunguzi katika afisi ya ardhi, na kujua ukweli wa mambo.

  • Tags

You can share this post!

Ngunjiri asalimisha bunduki yake kwa polisi

Wakazi wa Mokowe katika kaunti ya Lamu wakabiliwa na uhaba...

adminleo