• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
KANU yaanza kuchangisha pesa za kampeni za 2022

KANU yaanza kuchangisha pesa za kampeni za 2022

 SIMON CIURI na FAUSTINE NGILA

Chama cha KANU kimeanzisha mpango wa kutafuta pesa zitakzatotumika kwenye kampeni za 2022.

Chama hicho kilisema kwamba kimeamua kuuzua mali yake ya thamna ya Sh1.3 milioni ili kuongeza kiwango cha fedha.

Bw George Wainaina, ambaye ni katibu wa chama cha KANU pamoja na mwenyekiti wa KANU Kiambu alisema kwamba pesa hio itatumika kuimarisha shughuli za chama.

“Ripoti zetu zinaonyesha kwamba tuna mali ya Zaidi ya Sh 1.3 bilioni ambayo imekuwa ihatumiki na imekua ikitumiwa vibaya kwa miaka mingi.

“Mali hio ni pamoja na nyumba na mashamba.Tumeteua agentiambaye atauza mali hio kwa niaba yetu.Tutatumia pesa hio kuimarisha shughuli za chama chetu,”Bw Wainaina aliambia Taifa Leo.

“Agenda yetu kwa sasa ni kukipigia ndebe chamba chetu nchi mzima na tunataka fedha za kuendesha shughuli hiyo.”

Bw Wainaina alisema kwamba chama hicho kinasajili wanachama wapya kwasababu watasimamisha mgombea wa urais mwaka 2022.

“Ili hii iwezekane iwezekane lazima tuwe na pesa za kutosha.”

Bw Wainaina alisema kwamba swala hio ya kuuza baadhi ya mali ya KANU ilidhinishwa na mwenyekiti wa chama hicho Gideon Moi.

Mali mingi ambayo tunauza iko,Nairobi,Mombasa,Kisumu,Kiambu na Bonde la Ufa.

  • Tags

You can share this post!

Mahakama mbili zafungwa kwa sababu ya corona

Shule mitaani sasa zakodishwa