Habari Mseto

Kaunti nane kukosa umeme Kenya Power ikiboresha mfumo wake

January 25th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA WANDERI KAMAU

KAMPUNI ya Kenya Power imetangaza kwamba kaunti nane katika maeneo manne zitakosa umeme nyakati tofauti Alhamisi.

Kwenye taarifa, kampuni ilisema kuwa kaunti hizo zitakosa umeme nyakati tofauti za siku.

Kaunti zitakazokosa huduma hizo ni Nairobi, Machakos, Kajiado, Murang’a, Trans Nzoia, Homa Bay, Mombasa na Kilifi.

Katika Kaunti ya Nairobi, baadhi ya maeneo yaliyolengwa yatakosa umeme kati ya saa 3.00 asubuhi na saa 11.00 alasiri.

Baadhi ya maeneo yatakayokosa umeme jijini ni barabara ya Kibagare Way, mtaa wa Kibagare na maeneo yaliyo karibu.

Katika Kaunti ya Machakos, huduma za umeme zitakosekana kati ya saa 3.00 asubuhi na saa 11.00 jioni. Maeneo hayo yanajumuisha Quickmart Express, Grogon, Machakos Girls, Five Hills, Misakwani, Kyambuko, Westgate na Milima ya Iveti.

Katika Kaunti ya Kajiado, maeneo yaliyolengwa yatakosa umeme kati ya saa 2.00 asubuhi na saa 11.00 jioni. Maeneo hayo ni Sajiloni, Enkorika, Enduata, Ol Kejuado School, Kipeto, Oloosuyian, Kikayaya, Hospitali ya Rufaa ya Kajiado kati ya maeneo mengine.

Katika Kaunti ya Murang’a, maeneo yatakayoathiriwa ni mitaa ya Branan, Bedor, Githumbuini, Golden Pearl, Soko la Kahaini, Geroge Thuo & OLA, Ngararia Girls na Ngararia Mkt, Kiunyu, Kiama Est, Gatoka, Gatunyu, Kimatus, Mabanda, Ithangariri, Gatanga, Kirwara, Gateiguru, Mukarara, Rugaita, Kihumbuini, Thuita, Mukurwe, Njaini Mkt, Naaro, Muruka na Kiranga.

Kampuni hiyo imekuwa ikiendesha shughuli za kuboresha mfumo wake wa usambazaji umeme.