• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Kaunti ya Samburu yageukia maombi ili kukabili ujangili

Kaunti ya Samburu yageukia maombi ili kukabili ujangili

NA GEOFFREY ONDIEKI

UTAWALA wa Kaunti ya Samburu sasa umeamua kugeukia maombi kama njia ya kukomesha ujangili ambao umesababisha vifo vya raia wengi wakiwemo maafisa wa usalama.

Visa vya wizi wa mifugo, mashambulio na uharibifu wa maji vimevuruga hali ya maisha katika kaunti hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Baada ya juhudi za maafisa wa usalama za kukomesha hali hii kutozaa matunda, Gavana wa Samburu, Lati Lelelit, sasa anaandaa maombi yanayoshirikisha makanisa mbalimbali na viongozi wa eneo hilo kuombea amani.

“Tunahisi ni muhimu kuandaa maombi ili kukomesha hali hii. Tayari tumewaarifu viongozi wetu wa kidini kwamba tutawahitaji kuongoza maombi hayo. Tunahisi kuwa kutafuta usaidizi wa Mungu wakati kama huu kutatuwezesha kupata amani,” akasema.

Mwenyekiti wa Baraza la Kitaifa la Makanisa Nchini (NCCK) Kaunti ya Samburu, Askofu Joram Kiarie juzi alisema kuwa kudorora kwa hali ya usalama katika katika kaunti hiyo kunahitaji hatua madhubuti kutoka kwa serikali.

Kiarie ambaye ni Askofu wa Kanisa laPentecoal Evangelist Fellowship aliishauri serikali kushirikiana na makanisa kuanzisha mazungumzo kwa lengo la kukomesha msururu wa mashambulio katika maeneo kadhaa ya Kaskazini mwa Bonde la Ufa.

Kiongozi huyo wa kanisa alisema kuwa wakazi wanateseka kutokana na mashambulio ya kila mara ambayo yamechangia maafa makubwa na uharifu wa mali ya thamani kubwa.

“Viongozi wanafaa kuongoza mazungumzo ya kuleta maridhiano miongoni mwa jamii zinazozona. Kanisa liko tayari kuongoza mchakato huu wa maridhiano ili kurejeshe amani katika eneo hili,” akasema Askofu Kiarie.

  • Tags

You can share this post!

Man United walivyoponea kupigwa rungu na limbukeni Coventry...

Spika wa Bunge aliyeanza maisha kama ‘beach boy’

T L