• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
KCSE: Walimu 15 kusalia ndani kwa wiki mbili

KCSE: Walimu 15 kusalia ndani kwa wiki mbili

Na JADSON GICHANA

WALIMU kumi na watano ambao walishikwa wiki moja iliyopita kwa kupatikana na maswali ya mtihani wa KCSE kinyume cha sheria watasalia gerezani kwa siku kumi na nne zijazo.

Washukiwa hao akiwemo Mwalimu Mkuu na Naibu wake wa shule ya Sekondari ya Monianku,Msimamizi wa mtihani huo na walimu wasaidizi katika usimamizi huo.

Walimu hao ni Irene Kivunja, Judith Nyaboke, Marori Edwin, Alex Ziko, Chrispers Ogora, Abuta John walipatikana na karatasi ya KCSE 233/1 ya Kemia Novemba 5, 2018 katika shule ya Sekondari ya Monianku,Kaunti ndogo ya Gucha,Kaunti ya Kisii kinyume cha sheria.

Katika shtaka la pili Motende John,Abuta John,Benard Omworo,Omgwa Joel Joel Nyakwanya Gedion Nyagaka, Edna Bitutu, Peter Arori Chritopher Otieno na Ann Nyaboke walipatikana wakiwa wanamiliki karatasi hiyo kinyume cha sheria za Baraza la mtihani nchini (KNEC) 2012 katika kipengele 27(3)

Katika shtaka la tatu Irene Kivunja, Judith Nyaboke, Marori Edwin, Alex Ziko,Chrispers Ogora,Abuta John, Peter Arori, Christopher Otieno na Judith Nyaboke walishtakiwa kwa kusaidia katika wizi huo kinyume cha sheria katika Baraza la usimamizi wa mtihani (KNEC)2012 sehemu 40.

Mnamo novemba 5,2018 katika shule ya Sekondari ya monianku,Kaunti ndogo ya Gucha, Kaunti ya Kisii kwa pamoja walitenda kitendo hicho kwa kujaza majibu kwenye karatasi hilo la mtihani wa KCSE Kemia (1).

Walikabiliwa na mashtaka matatu ya kupatikana na karatasi hilo nje ya shule katika boma moja.

Washukiwa hao walinyimwa dhamana na Hakimu Mkaazi wa Ogembo Margaret Nafula kufuatia mafanikio ya maombi kutoka kwa upande wa mashtaka.

“Ninaamuru washukiwa hawa kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Nyamarambe hadi Novemba 29,2018 ndio nitafanya uamuzi,”alisema Hakimu huyo.

Akiwazilisha maombi yake mahakamani kiongozi wa mashtaka Peter Wainaina alisema kuwa kama washukiwa hao wataachiliwa kwa dhamana basi kuna uwezekano wataingilia mashahidi.

Waliwakilishwa na mawakili Kerosi Ondieki, Nyambega Mose, Sonye Ondari na Stephen Omwega walikana mashtaka hayo mbele ya Bi Nafula.

“Ninaomba mahakama hii kuwazuilia washukiwa hawa katika kituo cha polisi cha Nyamarambe kwa sababu wakiachiliwa kwa dhamana kuna uwezakano wa kuendelea kudanganya,”alisema Bw Wainaina.

Bw Wainaina alisema kuwa baadhi ya washukiwa hao hawakuwa na ajira ya kudumu na wakosa kuhudhuria mahakama.

Mahakama hiyo itatoa uamuzi kuhusu kesi Novemba 29, mwaka huu.

  • Tags

You can share this post!

SHERIA BARABARANI: Hatia za trafiki zitakazowatupa seli...

Mahindi: Peter Kenneth arai wakulima wakatae bei duni

adminleo