Habari Mseto

Kenya ina mabilionea 180 na mamilionea 1290 – Knight Frank

March 14th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Licha ya wananchi wengi kulalamikia hali ngumu ya maisha, Kenya ilipata milionea wapya 2017.

Kulingana na ripoti kuhusu utajiri ya Knight Frank, nchini kuna mamilionea wengine 180, ambapo idadi ya jumla ya milionea nchini sasa imefikia 1,290.

Ripoti hiyo imeorodhesha Wakenya walio na mapato ya Sh500 milioni na zaidi.

Licha ya uhaba wa chakula na siasa, kundi hilo halikuathirika. Mwaka wa 2016, Kenya ilikuwa na milionea 1,110 na idadi ya sasa ni ongezeko la asilimia 16.2, ilisema ripoti hiyo.

90 kati yao walikuwa na thamani ya zaidi ya Sh5 bilioni, chini ya 10 walikuwa na thamani ya Sh50 bilioni, ilieleza.

Katika muda wa miaka mitano ijayo, wananchi walio na thamani ya zaidi Sh500 milioni wataongezeka hadi 2,070, ongezeko la asilimia 74.

Milionea walibainishwa kuwa katika sekta za biashara, fedha, benki na uwekezaji pamoja na viwanda na utengenezaji wa bidhaa.