• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Kenya kufaidi kutokana na chanjo nafuu ya corona

Kenya kufaidi kutokana na chanjo nafuu ya corona

Na CHARLES WASONGA

KENYA imeorodheshwa miongoni mwa mataifa 92 masikini ambayo yatafaidi kutoka na chanjo mpya dhidi ya Covid-19 ambayo imevumbuliwa.

Tangazo hilo limetolewa na Shirika la Global Vaccine Alliance (Gavi) ambalo linashirikisha wadau kutoka sekta ya umma na kibinafisi, na ambalo linafanya mazungumzo na kampuni mbalimbali za kutengeneza chanjo, kwa niaba ya nchi masikini zilizoathirika zaidi na janga la corona.

Kulingana na Gavi, chanjo hiyo itagharimu Sh300 kwa kipimo kimoja katika mataifa hayo masikini.

Mataifa mengine ambayo yatafaidi chini ya mpango huo ni Cameroon, Nigeria, Zambia, Ghana, India, Misiri, Lesotho, Ethiopia, Sudan Kusini, kati ya mengine.

“Sasa tumeweka mpango wa kuhakikisha kuwa kila nchi, haswa zile masikini haziachwi nyuma nje ya mataifa yatakayofaidika na chanjo ya Covid-19,” akasema afisi mkuu Dkt Seth Berkley kwenye taarifa katika tovuti ya shirika la Gavi

Kulingana na shirika hilo linalenga kuhakikisha kuwa kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2021 litakuwa limewasilisha vipimo bilioni 2 vya chanjo katika mataifa yote.

Baada ya chanjo kuidhinishwa na mashirika ya kubaini ubora pamoja na shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), chanjo hizo zitanunuliwa na kisha kusambazwa.

Gavi itafanyakazi na serikali, mashirika ya kimataifa, watengenezaji chanji na mashirika ya umma kuhakikisha kuwa dawa hizo zinafikia wale wanaozihitaji,” akasema Berkley.

Wakfu wa Belinda Gates na shirika la Gavi zimeitwika Taasisi ya Serum Institute ya India (SII) wajibu wa kutengeneza vipimo 100 milioni za chanjo faafu na salama ya Covid-19 kwa ajili ya mataifa masikini kuanzia 202.

Miongoni mwa chanjo ambazo taasisi ya SII itatengeneza ni “ChAdOx1” inayotengenezwa na kampeni ya AstraZeneca na “NVX-CoV2373” inayotengenezwa na kampuni ya Novavax.

You can share this post!

Matiang’i afanya mabadiliko katika utawala wa mkoa

Nyumba 100 zateketea Mukuru