• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 7:47 PM
Kesi dhidi ya Wazir Chacha yaunganishwa na nyingine

Kesi dhidi ya Wazir Chacha yaunganishwa na nyingine

Na RICHARD MUNGUTI

KESI dhidi ya mwanaume anayedaiwa alikuwa akipokea pesa kutoka kwa Wabunge akijifanya kuwa Mwakilishi Mwanamke wa Kaunti ya Murang’a Bi Sabina Wanjiru Chege imeunganishwa na nyingine ambapo washukiwa wengine wameshtakiwa.

Bw Waziri Benson Masubo Chacha (pichani) alikanusha mashtaka sita mbele ya hakimu mkuu katika mahakama ya Nairobi Bi Rosline Oganyo

Wakili Job Ngeresa anayemtetea mshtakiwa aliomba Bw Chacha aliyetiwa nguvuni nchini Tanzania akitoroka aliomba aachiliwe kwa dhamana.

Bw Ngeresa aliomba mahakama ishurutishe afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma  (DPP) imkabidhi nakala ya ripoti ya mshtakiwa kutoka hospitali ya kutibu wenda wazimu ya Mathare ambapo Bw Chacha alipelekwa kupimwa ikiwa akili yake ni timamu.

Pia, Bw Ngeresa aliomba korti imwachilie mshtakiwa kwa dhamana akisema ni haki yake ya kikatiba kupewa dhamana ndipo afanye kesi akiwa nje.

“Naomba hii mahakama iamuru upande wa mashtaka unikabidhi nakala za mashahidi ndipo mshtakiwa aandae ushahidi wake wa kujitetea,” aliomba Bw Ngeresa.

Lakini kiongozi wa mashtaka Bw Solomon Naulikha alisema atapinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana.

Mahakama ilifahamishwa kesi hiyo itaunganishwa na nyingine ambapo muuzaji katika duka la Mpesa la Safaricom aliyedaiwa alisajili nambari ya Bi Chege kwa jina la Bw Chacha ameshtakiwa.

Bw Oganyo aliamuru mshtakiwa azuiliwe rumande hadi leo atakapofikishwa katika mahakama ya Citi kuwasilisha upya ombi lake la kuachiliwa kwa dhamana.

Shtaka la kwanza dhidi ya mshtakiwa lasema kwamba mnamo Machi 3 2018 katika duka la kuuza bidhaa za urembo ijulikanayo Update Beauty Shop iliyoko mtaa wa Donholm Nairobi akishikirikiana na watu wengine ambao aliandikisha  nambari ya simu nambari 0727008230 ya Bi Chege kwa lengo la kuwapunja wabunge na wananch

You can share this post!

Maraga: Najua Wakenya wamechoka lakini nina imani Uhuru...

JUNI 3: Tarehe ambayo Kenya itasafirisha mafuta ya kwanza...

adminleo