Kijana azikwa hai baada ya kuporomokewa na mgodi
GEORGE MUNENE NA FAUSTINE NGILA
Kijana wa miaka minane aliazikwa akiwa hai na mchanga baada ya mgondi kuporomoka Kijiji cha Kwavii Kaunti ya Kirinyaga.
Kijana huyo alikuwa ameandamana na mamayake Susan Muthoni ambaye bufanya kazi kwenye mgondi huo wakati tukio hilo lilitokea ambalo liliacha wanakijiji na msangao mkubwa.
Kulingana na walioshuudia kisa hicho Ian Mureithi aliacha mamayake ambaye alikuwa akigoga mawe na kuanza kuchzea karibu na mgondi.
Mara hio hio mgondi huo uliporomoka na ukamzika akiwa hai.
“Upande wa juu wa mgondi huo uliporomoka huku ukimzika kijana huyo aliyekuwa akichezea eneo hilo,”alisema shahidi aliyeshuudia kisa hicho.
Mama ya mwendazake alisema kwamba alisikia mtoto wake akilia na akakimbia kwenye eneo la tukio hapo ndipo alipata mwanawe akiwa amefunikiwa na mawe.
Alipiga duru huku wafanyakazi wezake wakiitikia wito wake .Walijaribu kuokoa kijana huyobila mafanikio.
“Tulijaribu kuokoa Maisha ya mwanangu bila mafanikio,”alisema mama huyo.
Mkuu wa polisi wa Mwea MagharribiAden Alio alisema kwamba walituma maafisa wa polisi kwenye eneo la tukio haraka iwezekanavyo na kisa hicho kikaripotiwa kwa polisi.
“Timu ya uokoaji lilikuwa na wakati mgumu kutoa mwili wa kijana huyo kwani ulikuwa umefunikwa na mawe,”alisema Bw Alio.