Habari Mseto

KJMA yakemea wanaokejeli Idara ya Mahakama

January 25th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na RICHARD MUNGUTI

CHAMA cha Mahakimu na Majaji (KJMA) Ijumaa kilijitenga na lawama kwamba Idara ya Mahakama imekuwa kizingiti katika vita dhidi ya ufisadi.

KMJA kilisema kuwa idara ya mahakama imesimama kidete kupigana kufa kupona na ufisadi sawia na kutekeleza majukumu yake ya kikatiba kwa mujibu wa Kifungu nambari 160 (1) cha Katiba.

Katika taarifa iliyotolewa katika mahakama ya Milimani Nairobi ,KMJA kilisema kuwa “ Majaji na Mahakimu hawatalengeza kamba katika kupambana na ufisadi.” Kiliwataka wananchi wasiangukie mitego ya wahongo na badala yake wafike kortini kupata huduma kwa njia ya haki na utendevu.

Kilisema kuwa vita dhidi ya ufisadi havitashindwa kwa kujitukuza ama kujipiga kifua mbali itategemea ushahidi na ukakamavu wa kuwachunguza washukiwa

Chama hicho kiliwalaani baadhi ya viongozi wakuu serikalini ambao wamekuwa wakilaumu idara ya mahakama , majaji na mahakimu wakidai .” imekuwa kizingiti katika vita dhidi ya ufisadi.”

KMJA kiliwataka viongozi wakome kuingilia idara ya mahakama kikisema majaji na mahakimu hutegemea ushahidi unaowasilishgwa na afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuamua kesi za ufisadi.

“Mahakama imewaadhibu washukiwa kadhaa na inaendelea kusikiza kesi nyingine za ufisadi licha ya changamoto za

“ Idara ya mahakama ni huru, haipasi kupata maagizo kutoka kwa mtu au idara yeyote. Inaamua kesi kulingana na ushahidi unaowasilishwa na afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP),” alisema Katibu Mkuu wa KMJA Bw Derick Kuto.

Katika taarifa iliyotiwa saini ni mwenyekiti wa KMJA Jaji Jacqueline Kamau, chama hicho kiliwasihi viongozi wakome kuilaumu idara ya mahakama katika vita dhidi ya ufisadi.

“Idara ya mahakama imejitolea kupambana na ufisadi na imewaadhibu washukiwa wanaopatikana na hatia ya ufisadi na kuwaachilia ambao hakuna ushahidi wa kutosha katika kesi zinazowakabili,” alisema Jaji Kamau.

“Tunawahakikishia wananchi kuwa idara ya mahakama imejitolea kupambana na ufisadi kwa kuwasukuma jela wanaopatikana na hatia ya kuhusika na ufisadi,” KMJA kilisema.