• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Korti yasitisha mazishi kutokana na mzozo wa ardhi

Korti yasitisha mazishi kutokana na mzozo wa ardhi

GEORGE MUNENE NA FAUSTINE NGILA

Waombolezaji walipigwa na butwaa wakati mazishi ya mwanamke mmoja yalisimamishwa Kijiji cha Kiamugumo Kaunti ya Kirinyanga kufuatia amri ya Korti.

Waombolezaji hao walikuwa wamekutana ili kumpa Bi Saraha Wambui wa miak 41 mkono wa buriani wakati amri hiyo ya korti ilipeanwa huku ikiwazuia kumzika mwanao kwa madai ya mzozo wa ardhi.

Hisia za waatu ailipanda njuu wakati familia ilitangaza kwamba mazishi hayo hayawezi kuendelea kwani korti ilikuwa imesimamishwa na korti.

Matayarisho yote ya mazishi yalikuwa yamekamilika wakati Nancy Njoki ambaye anadai umiliki wa kipande hicho chaardhi ambacho Bi Wambui alikuwa azikwe alifika na amri hiyo ya korti.

Bi Njoki alilaumu familia ya Wambui kwa kutaka kumzika mwanao kwa arhi yake bila kmjulisha.

Amri hiyo ya korti ilizuia familia ya mwendazake kumzika kwenye kipande cha ardhi ambacho kilikuwa na mzozo mpaka kesi iliyoandikishwa na njoki isikizwe.

Mamayake Wambui  Esther Gutu alisema kwamba amri hiyo ya korti iliwashangaza.

“Tulishangazwa  na amri hiyo ya korti ya kusimamisha mazishi yaWambui ambaye alifariki baada ya kuungua kwa muda mfupi”alisema Bi Gutu.

Bi Gutu alisema kwamba mwanawe aliishi kwa shamba hilo kwa muda mrefu na kwamba familia haipaswi kuzuiliwa kuzika  mwananwe.

“Hata mumewe alizikwa kwenye ardhi hiyo  bila mtu yeyote kulalamika,”alisema Bi Gutu.

  • Tags

You can share this post!

AKILIMALI: Mwalimu anayetambua umuhimu wa ufugaji na...

Washangaa kupata mwili uliochomwa wa mwanamke chumbani...