• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 4:42 PM
KPC yapiga jeki uhifadhi wa misitu Mombasa

KPC yapiga jeki uhifadhi wa misitu Mombasa

NA WINNIE ATIENO

KAMPUNI ya Kenya Pipeline (KPC) kwa ushirikiano na Huduma za Misitu Nchini (KFS) imetia saini mkataba wa maelewano kuhifadhi misitu ya umma na ulinzi wa mabomba ya mafuta kwenye maeneo ya hifadhi za misitu.

Akizungumza wakati wa upanzi wa mikoko eneo la Jomvu, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Kenya Pipeline, Bw Joe Sang alibainisha kuwa wanalenga kukuza miti milioni tano katika muda wa miaka kumi ijayo taifa zima.

Mashirika hayo ya kiserikali yalipanda miche 440 ya mikoko.

“Mradi huu wa upanzi wa miti utasaidia pia nafasi za ajira kando na kuhifadhi mazingira. Vijana ambao wanajihusisha na uhifadhi wa mikoko wataweza kufuga nyuki ili wapate asali,” alisema Bw Sang.

Bw Sang alipongeza KFS kwa juhudi zake za uhifadhi wa misitu.

 

  • Tags

You can share this post!

Wakataa barabara kupitia hifadhi ya wanyama pori

Migodi ya dhahabu ilivyogeuka kuwa ngome ya mauti 

T L