Habari Mseto

KRA kuwatuza walipa ushuru bora zaidi

October 31st, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Mamlaka ya Kukusanya Ushuru nchini (KRA) itawatuza walipaji bora wa ushuru nchini Jumatatu katika hafla itakayofanyika katika Jumba la Kibiashara la Kenyatta (KICC).

Hafla hiyo hufanywa kila mwaka na watakaotuzwa mwaka huu ni wale wametii na kulipa ushuru kwa wakati unaofaa mwaka wa 2017.

Sherehe hiyo itaongozwa na Rais Uhuru Kenyatta na Waziri wa Fedha Henry Rotich na Mwenyekiti wa Bodi ya KRA Francis Muthaura, kamishna wa KRA na wengine kutoka sekta ya umma na sekta ya kibinafsi.

Wakati huo, KRA itazindua kituo cha skana tangamani na usimamizi, ambao ni mfumo wa kidijitali ambao unaunganisha skana za KRA kwa lengo za kuangalia jinsi zinavyofanya kazi.

“Uzinduzi wa kituo hicho ni muhimu kwa sababu utasaidia kuimarisha operesheni forodhani hasa katika kugundua baadhi ya bidhaa na kusaidia kulinda mipaka,” ilisema KRA katika taarifa Jumatano.

Pia, kitazinduliwa kwa lengo la kuimarisha operesheni na kukuza biashara kati ya mataifa.