Habari Mseto

KRA yalenga kukusanya Sh2 bilioni kwa wenye biashara ndogo

January 9th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

MAMLAKA ya Kukusanya Ushuru nchini (KRA) inalenga kukusanya Sh2 bilioni kwa mwaka kutoka kwa wafanyabiashara wadogo.

Hii ni baada ya serikali kuanza kutekeleza ushuru mpya. KRA ilisema inashirikiana na simamizi za kaunti kuisaidia kukusanya ushuru huo unaolenga wafanyibiashara wadogo ambao hupata hupata chini ya Sh5 milioni kwa mwaka.

Wafanyibiashara wa jua kali wanafaa kulipa ushuru wa asilimia 15 ada ya biashara moja ambayo hutolewa na serikali za kaunti wanapoenda kufanya upya leseni zao kuanzia mwezi huu.

“KRA inalenga kukusanya Sh2 bilioni kufikia mwishoni mwa mwaka huu wa kifedha,” alisema kamishna wa KRA anayesimamia ubunifu na hali hatari Mohamed Omar.

Lakini huenda utekelezaji wake haujaanza vilivyo hasa kutokana na kuwa wafanyibiashara bado hawajui kuhusiana na ushuru huo.