• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 5:01 PM
KRA yalenga kuongeza kiwango cha mapato 2019

KRA yalenga kuongeza kiwango cha mapato 2019

Na BERNARDINE MUTANU

Mamlaka ya Utozaji Ushuru (KRA) linalenga kuongeza kiwango cha mapato kutoka asilimia 18.3 katika mwaka wa kifedha wa 2017/2018 hadi asilimia 19.2 katika mwaka wa kifedha wa 2020/2021.

Kupitia kwa mpango wake wa saba wa usimamizi kutoka 2018-2021, KRA inalenga kupata Sh6.1 trillioni.

Mamlaka hiyo inalenga ukuaji wa asilimia 12.9 kwa mwaka kwa lengo la kuwa na uwezo wa kuokota kiasi hicho cha fedha.

KRA inalenga kupanua maeneo ya kupata ushuru ikiwemo ni pamoja na kupata walipaji ushuru kutoka 3.94 milioni hadi milioni saba kwa kukusanya ushuru kuambatana na sekta.

Wakati wa uzinduzi wa mpango huo na Waziri wa Fedha Henry Rotich, usimamizi wa KRA ulisema mwongozo huo utaiwezesha kukusanya ipasavyo.

“Ninaamini juhudi nyingi ziliwekwa katika kubuni mpango huu unaotarajiwa kuwa muhimu sana katika utekelezaji wa Big 4 Agenda,” alisema Bw Rotich.

You can share this post!

Sylvia Kamau ateuliwa kusimamia KRU

KEPSA yakemea vikali mauaji ya 14 Riverside

adminleo