Habari Mseto

KRA yawataka wanachuo kuwasilisha taarifa za ushuru kidijitali

February 23rd, 2019 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

TANGU Mamlaka ya Ukusanyaji wa Ushuru (KRA) ilipofungua nafasi ya kujaza ushuru kwa mwaka wa 2018, takriban Wakenya 3.2 milioni wameandikisha ushuru kwa mapato yao.

KRA wakati huo imewataka wananchi kuandikisha ushuru wao kwa wakati ufaao kuepuka kutozwa faini.

Katika taarifa, shirika hilo lilisema kuwa limeimarisha mfumo wake wa kuandikisha ushuru na kufanya rahisi kuandikisha kwa kutumia mtandao.

Hata wanafunzi wa vyuo vikuu walio na nambari ya utambulisho (PIN) watahitajika kujaza mtandaoni ushuru kutokana na mapato yao hata kama hawana.

“Wote walio na PIN na wasio na mapato, kwa mfano, wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za mafunzo watahitajika kujaza ‘NIL returns’.”

Siku ya mwisho ya kuwasilisha ushuru itakuwa ni Juni 30, 2019. Watakaotuma wakiwa wamechelewa watatozwa faini ya Sh2,000 kwa watu binafsi na Sh10,000 kwa kampuni au asilimia tano ya ushuru waliofaa kulipa.