Habari Mseto

Kuchelewa kwa mvua kutaibua baa la njaa nchini

February 21st, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Kiwango cha mvua kinatarajiwa kuwa chini katika msimu wa mvua inayotarajiwa kati ya Machi na Mei katika maeneo mengi nchini.

Hii ni kumaanisha kuwa watu wanatarajia kukabiliwa na njaa kutokana na mazao yaliyopungua.

Idara ya utabiri wa hali ya hewa Jumatatu ilisema kuwa baadhi ya maeneo yatapata mvua iliyochelewa, hali inayotarajiwa kuathiri upanzi wa mimea na mavuno.

Hata hivyo, maeneo ya Magharibi mwa Kenya, Bonde la Ufa katikati, sehemu za Kati na Nairobi, yatapata karibu kiwango cha kawaida cha mvua.

“Maeno mengi yatakuwa kame kabla ya msimu wa mvua ya masika inayotarajiwa kuanza mwezi ujao,” alisema afisa wa Idara ya Kutabiri hali ya Hews Peter Ambenje.

Katika maeneo kunakotarajiwa mvua kubwa, huenda kukawa na mafuriko, alisema.