• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 3:16 PM
Kutanyesha tena, yasema idara

Kutanyesha tena, yasema idara

Na BERNARDINE MUTANU

Mvua inatarajiwa kurejea maeneo kadhaa nchini kwa mujibu wa idara ya hali ya hewa nchini.

Jumatano, idara hiyo ilitangaza kuwa mvua kubwa inatarajiwa maeneo ya magharibi ingawa maeno ya kaskazini yatasalia makavu na yatakuwa na joto.

Maeneo yanayotarajiwa kuwa na mvua kwa muda wa wiki moja ijayo ni karibu na Ziwa Victoria, maeneo ya juu Bonde la Ufa na Pwani.

Maeneo ya Siaya, Kisumu, Homa Bay, Migori, Kisii, Nyamira, Trans Nzoia, Baringo, Uasin Gishu, Elgeyo-Marakwet, Nandi, Laikipia, Nakuru, Narok, Kericho, Bomet, Kakamega, Vihiga, Bungoma na Busia yatashuhudia mvua wakati wa jioni, itakayoandamana na ngurumo za radi.

Kulingana na mkurugenzi wa idara hiyo Peter Ambeje, maeneo ya Nairobi na Kati yatasalia baridi na kutakuwa na mawingu kwa muda wa siku saba zijazo.

Ripoti ya idara hiyo inaonyesha kuwa kwa muda wa wiki moja ijayo, maeneo ya Mombasa, Tana River, Kilifi, Lamu na Kwale yatashuhudia mvua isiyo kubwa wakati wa asubuhi kati ya Alhamisi na Jumamosi.

You can share this post!

Oserian yachunguzwa kwa kuwakandamiza wafanyakazi wa maua

FKE yapinga wafanyakazi kutozwa ada ya kujenga nyumba

adminleo