• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 1:13 PM
Linah Anyango ateuliwa kuwania tuzo ya mwalimu bora duniani

Linah Anyango ateuliwa kuwania tuzo ya mwalimu bora duniani

Na MAGDALENE WANJA

MWAKA mmoja tu baada ya mwalimu Peter Tabichi kushinda tuzo ya mwalimu bora duniani, mwalimu mwingine kutoka nchini Kenya ameteuliwa kuwania tuzo hiyo ya hadhi.

Bi Linah Anyango ambaye ni mwalimu wa masomo ya biolojia na kemia katika shule ya upili ya Changamwe ni miongoni mwa walimu 50 wa kwanza katika uteuzi huo.

Bi Anyango aliteuliwa na ni miongoni mwa walimu 12,000 kutoka nchi 140 kote duniani wanaowania tuzo hiyo.

Tuzo hiyo ya Sh100 milioni iko katika mwaka wake wa sita tangu kuanzishwa kwake.

Ilianzishwa ili kuwatambua walimu ambao wana ubunifu na ambao wamechangia kwa njia ya kipekee katika kazi yao.

Tuzo hilo lilianzishwa ili kuwatambua walimu ambao Wana ubunifu na ambao wamechangia kwa kipekee katika kazi yao.

Bw Tabichi ambaye alipokea tuzo hiyo mwaka 2019 ameelezea furaha yake kuwa mwalimu mwingine kutoka nchini Kenya amepata nafasi nzuri ya kuwania tuzo.

“Najivunia kuwa mwalimu kutoka Kenya ameteuliwa katika tuzo ya mwaka 2020. Namtakia Bi Linah Anyango kila la heri,” amesema Bw Tabichi.

  • Tags

You can share this post!

Wenye magari ya uchukuzi waagizwa kuweka orodha ya abiria...

Wauguzi wataja nyenzo muhimu kwao kukabiliana na Covid-19

adminleo