• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 8:50 AM
LSK yataka maagizo ya idara kusimamiwa na AG yafutwe

LSK yataka maagizo ya idara kusimamiwa na AG yafutwe

Na RICHARD MUNGUTI

CHAMA  cha wanasheria nchini LSK kimewasilisha kesi ya kupinga agizo la Rais Uhuru Kenyatta  la kuweka tume na idara huru chini ya usimamizi wa afisi ya mwanasheria mkuu (AG).

LSK kimemshtaki AG kikiomba maagizo hayo ya Rais Kenyatta yafutiliwe mbali.

Wakili Miller Bwire aliyewasilisha kesi hiyo chini ya sheria za dharura alisema tume huru na idara zilizopewa mamlaka na Katiba zimekandamizwa kwa kuwekwa chini ya usimamizi na kuthibitiwa na AG.

LSK kimesema kuwa agizo hilo la Rais Kenyatta ni njia ya kubadilisha katiba kwa vile mwanasheria mkuu sio Waziri aliyeteuliwa kwa mujibu wa katiba.

“Agizo hilo la Rais Kenyatta inakinzana na katiba na yapasa kupigwa kalamu,” alisema Bw Bwire.

Aliongeza: “Naomba mahakama  isitishe kutekelezwa kwa agizo hili inayokinzana na vipengee vya katiba.”

Chama hiki kimeorodhesha tume 20 pamoja na idara za Serikali zilizowekwa chini ya usimamizi wa AG

Baadhi ya idara zilizowekwa chini ya usimami wa AG ni pamoja na Afisi ya Mkurugenzi wa mashtaka ya umma DPP.

Mbali na afisi ya AG baadhi ya idara na tume zimewekwa chini ya afisi  ya Rais , Wizara za Elimu, Ardhi na Utumishi wa Umma, Vijana na Masuala ya Jinsia.

Tume hizo ni  Tume ya kitaifa  Kubadili Sheria (KLRC), Baraza la Masuala ya Sheria (CLE),,Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (RPP),Mamlaka ya Kurejesha Mali ya Umma iliyoibwa (ARA),Chuo cha Uanasheria (KSL), Bodi ya Haki za Bidhaa (KCB) , Bodi ya Kuwalinda wahasiriwa (VPB) , Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Binadamu (KNHRC).

Nyingine ni Tume za Haki na Usimamizi , Tume ya kuajiri Watumishi wa Idara ya Mahakama, T ume ya Bunge, Huduma za Polisi, Tume ya ukusanya ushuru (CRC), tume ya mishahara (SRC) . Tume ya kuajiri walimu (TSC). Tume ya kitaifa ya Ardhi (NLC)

  • Tags

You can share this post!

Mkono mrefu wa sheria wamkamatia nchini Sudan Kusini

Wawili washtakiwa kuiba Sh5 milioni

adminleo