• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Maandamano Kagwe na Wamalwa wakizuru Kakamega

Maandamano Kagwe na Wamalwa wakizuru Kakamega

BENSON AMADALA na FAUSTINE NGILA

Maandamano ya wafanyabiashara yalitatiza shughuli kwenye makao makuu ya Kaunti ya Kakamega wakati gavana Oparanya alikuwa anajitayarisha kumpokea waziri wa afya Mutahi Kagwe na mwezake wa ugatuzi Eugene Wamalwa.

Kizaazaa kilizuka wakati Gavana Oparanya aliondoka pamoja na waziri Wamalwa kutembelea kituo cha kuwatenga wagonjwa wa corona.

Wafanyabiashara waliokuwa na ghadhabu walifunga barabara kuu ya kuingia makao makuu ya kaunti hiyo wakilalamika kutekelezwa na kaunti hiyo, huku wakidai kwamba serikali hio hijawai kuwapa maski na viyeyuzi.

Bw Kagwe anatarajiwa kutembelea hospitali ya rufaa na mafunzo ya Kakamega kuchunguza jinsi kaunti hio imejitayarisha kupambana na virusi vya corona.

Gavana wa kaunti hio alikuwa tayari ameshapokea waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa na kiogozi wa wengi Emmanuel Wagwe ofisi kwake wakati kizaazaa hicho kilizuka.

Maandamano hayo yalichochewa na ubomoaji wa duka zilizokuwa zimejengwa karibu na barabara inayoelekea kwenye hospitali hio ya Kakamega ambapo Waziri wa afya alikuwa anatarajiwa.

 

  • Tags

You can share this post!

MUTUA: Uozo wa ajabu kugeuza corona kitega uchumi

Corona imeathiri Waafrika milioni 5